Nashauri wadau badala ya kusubiri serikali kurekebisha mkataba nendeni moja kwa moja UAE na mapendekezo ya marekebisho.
Na nina rudia UAE sio Dubai pekee maana tuna uhusiano na UAE kama nchi na sio Dubai. Lakini twende na mapendekezo kabisa ya marekebisho ya mkataba naamini kabisa wataaikiliza na kufanya marekebisho. Hii ni kwasababu serikali ya UAE haitapenda haya yanayoendelea.
Serikali inawezekana kuna waliokula pesa na ndiyo maana hawataweza kwenda kwa Dubai kusema malalamiko.
Si jukumu la wanaharakati kuomba marekebisho kwenye mkataba, walioingia mkataba wakidhani Tanzania haina watu wanaojali ndio wenye jukumu hilo, ila da! Zile gharama za wabunge na wasiojulikana waliokwenda kwenye shopping spree atarudisha nani.
Wewe ndiyo unajua kila kitu sheria zote na nini cha kufanya. Watanzania wengi ndiyo wanafikiria kama wewe!. Mimi ushauri wangu ni kwenda kuongea na wahusika kama wanaharakati! tatizo ni nini hapo