Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Hii hoja labda ingekuwa na mashiko kabla ya Lissu kugombea uenyekiti.ANAANDIKA MHADHIRI WA CHUO KIKUU TUMAINI DR DLB
“Kinachoniumiza ni baadhi ya wanaChadema kutoliona hili la wanaharakati ambao siyo wana Chadema ndiyo wanaongoza mapambano ya kutaka Mbowe atoke, njia ile ile iliyotumika na wanaharakati kuimaliza NCCR Mageuzi ndiyo inataka kutumika kuipasua Chadema.
Na bahati mbaya sana baadhi ya wanaChadema bila kujua wameamua kuungana na wanaharakati hawa ambao kila ukiwasikiliza unaona wanataka kugawana fito.
Wanaharakati hawa waliiua NCCR na kutokomea mbali,wakamfukuza mpaka Mbatia na leo wameshindwa kuinyanyua NCCR na badala yake wapo bize na Chadema huku wakiwateka watu wenye ushawishi ndani ya chadema .
Hawa wakishamuangusha Mbowe,ndani ya miaka miwili watatandikana viboko na kuiacha chadema ikiwa gofu”.
In fact, kabla ya Lissu kugombea uenyekiti, hata mimi nilisema watu wanaomtaka Mbowe aondolewe kwenye uenyekiti walikuwa hawana legitimacy katika chama, kwa sababu kwenye chama kulikuwa hakuna mtu aliyechukua fomu kumpinga Mbowe.
Baada ya Lissu kugombea uenyekiti, issue ya Mbowe kupingwa si ya wanaharakati wa mitandaoni tu, ni issue ambayo imekubalika mpaka na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA.
Kwa hivyo, msiidogoshe kusema ni ya wanaharakati tu.