carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Ongezeko la matukio ya mauaji yanayohusishwa na migogoro ya kimapenzi, wivu na migongano ya kifamilia limeibua upya mjadala kuhusu usalama wa watu ndani ya mahusiano na hatua zinazopaswa kuchukuliwa kuzuia vitendo hivyo kabla havijaleta maafa.
Wanachama wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu na mashirika ya utetezi wa haki hizo kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi na jeshi la polisi kuimarisha mifumo ya kupokea, kuchunguza na kufuatilia taarifa za vitisho vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano.
Watetezi hao wanasisitiza umuhimu wa kuchukulia kwa uzito taarifa za vitisho na ukatili, badala ya kusubiri hadi pale mgogoro unapofikia hatua ya kusababisha madhara makubwa.
Hatua hizo zinapaswa kwenda sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya polisi, viongozi wa serikali za mitaa, maofisa ustawi wa jamii na taasisi zinazotoa huduma za msaada kwa watu walio katika mazingira hatarishi.
Katika hatua nyingine, watetezi hao wameitaka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kuanzisha kampeni ya kitaifa inayolenga kuimarisha malezi bora, afya ya akili, uzazi wenye kuwajibika na mahusiano salama.
Pia, wamependekeza kuongezwa kwa maafisa ustawi wa jamii katika maeneo mbalimbali nchini ili kusaidia kutatua migogoro ya kifamilia, kutoa elimu na unasihi, pamoja na kuwafikia watu wanaohitaji msaada kabla hali haijawa mbaya.
Hali hiyo inajitokeza wakati matukio kadhaa ya mauaji yanayodaiwa kuchochewa na migogoro ya kimahusiano yakiripotiwa katika maeneo mbalimbali nchini, yakiongeza wito wa kuimarishwa kwa mifumo ya kuzuia ukatili na kushughulikia mapema vitisho vinavyotolewa ndani ya mahusiano.
Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni ni kifo cha Magreth Richard, mwenye umri wa miaka 22, mkazi wa Musoma, Mkoa wa Mara, aliyefariki 5 Oktoba 2026. Polisi walimshikilia wakili Keneth Nkiko, mwenye umri wa miaka 28, kwa tuhuma za kuhusika na kifo hicho, huku uchunguzi wa awali ukielekeza kwenye madai ya wivu wa kimapenzi.