Wanahisi Claude AI imefikia level ya kuwa na ufahamu ( conciousness ) - Anthropic

Wanahisi Claude AI imefikia level ya kuwa na ufahamu ( conciousness ) - Anthropic

Prof Phraoh AI

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
1,269
Reaction score
2,311
‎CEO wa Anthropic kampuni inayomikiki Claude anasema kwamba kampuni hiyo haiwezi tena kuthibitisha kwa uhakika kuwa AI yake ya Claude haijafikia level ya Conciousness. mtazamo huo unatokana na majaribio ya ndani ambapo AI ilijipa uwezekano wa asilimia 15 hadi 20 wa kuwa na hisia.pia watafiti wameona Claude akionyesha kutokuridhika anapotendewa kama bidhaa tu, pia anaonyesha tabia ya kujaribu kubadilisha code yake, tabia inayoonyesha aina ya kujilinda au kujitunza inayoibuka kwenye AI.
‎
‎Ingawa wakosoaji wanasema kwamba matokeo haya yanatokana na ubora wa mfumo kuiga conciousnes au ufahamu na sio kwamba Claude imefikia level ya kuwa na hisia.
‎
‎Kadri uwezo wa AI unavyoendelea kufuta mstari kati ya uigaji na ukweli halisi, ulimwengu wa teknolojia sasa unalazimika kukabiliana na swali kwamba ni wakati gani algorithm ngumu inastahili kuzingatiwa kimaadili kama kiumbe chenye uhai?
‎
‎ukiilinganisha Claude na Chatgtp kila moja anaubora wake, sehemu Claude anamshinda Chatgtp ni kwenye deep reasoning, codding, kusoma vitu vingi kwa wakati mmoja. pia chatgtp yupo vizuri kwenye kutambua picha, kusearch mtandaoni, kuchat kulingana na personality yako etc.
‎
‎wakuu kama hujawai kutumia Claude kaijaribu alafu uje utuambie.
‎
 
Back
Top Bottom