Wanaijeria walijisifu wanaijua biashara, Mchina kaingia maandamano yameanza “aondoke anaharibu biashara”

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736

Kwa miaka mingi, baadhi ya wafanyabiashara nchini Nigeria wamekuwa wakijisifu sana kuhusu umahiri wao katika biashara, wakijiona kama miongoni mwa wafanyabiashara hodari zaidi barani Afrika. Lakini baada ya “kisu kugonga mfupa” kutokana na ushindani mkali kutoka kwa wafanyabiashara Wachina, baadhi yao, hasa wafanyabiashara wa kabila la Igbo wenye maduka mengi nchini Nigeria, wameingia mitaani kuandamana.

Miongoni mwa hoja zinazotolewa ni kwamba:

  • “Mchina hatabakiza pesa Nigeria, atatuma sehemu kubwa kwao, wao wakipata pesa kwenye faida wanazitunza benki za Nigeria” huku hoja hiyo ikipuuzia kwamba biashara ni lazima zilipe kodi ambao wenyeji wamekuwa vinara wa kuzikwepa
  • Mchina anaua soko
  • Mchina atapunguza pesa kwenye mzunguko,
  • “Mchina haendi kanisani, hivyo hatatoa sadaka.”
  • Serikali inabidi iwalinde wafanyabiashara wanigeria
  • Na hoja nyingine kadhaa.
Kejeli kubwa ni kwamba wale waliokuwa wakijisifu kwa muda mrefu kuwa wanajua biashara na hawawezi kushindwa sokoni, sasa wanakutana na ushindani wa bei ambao umewalazimisha kuingia mitaani kulalamika.

Lakini hata hivyo, baadhi ya wateja wameonekana kupinga hoja za waandamanaji. Wamewalaumu baadhi ya wafanyabiashara wa ndani kwa kuwatoza bei kubwa kwa muda mrefu, wakisema bidhaa inaweza kununuliwa kwa bei fulani na kuuzwa kwa faida hata mara sita.

Kwa kifupi, wale waliokuwa wakisema “tunajua biashara” sasa wanaona upande mwingine wa biashara: ushindani.

Wachina wameanza pole pole ila wana mipango mikubwa sana, huko kwao Suppliers ni wengi sana wamestuka wanapoona wafanyabiashara wa Africa wakienda kununua kitu kwa bei ya chini ila wanakiuza kwa bei za juu sana Africa.

Maoni ya wasomi wa uchumi yanaonyesha vita hii ni ngumu sana, Mchina hanunui na kuuza tu, kaenda shule anajua kutengeneza anachouza (MANUFACTURING),
 
View attachment 3673643

View attachment 3673642

Afrika wafanya biashara ni wezi Sana🤣🤣
Bidhaa Ile Ile, Kodi Ile Ile, kiwanda lilelile lakini mchina anauza bei nafuu zaidi
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Hivi vipimbi kama kumi vimejikusanya kutengeneza mjengeo wa tiktok,
upuuzi mtupu
Nilidhani maandamano ya nchi nzima
 
Hili la wachina linahitaji DAWA!
... wanaleta ushindani usio na uwiano na kukata mitaji ya wazawa!
 
  • Kicheko
Reactions: Tsh
Hili la wachina linahitaji DAWA!
... wanaleta ushindani usio na uwiano na kukata mitaji ya wazawa!
Uwiano utaletwa kwa mchina kuuza bei kubwa sawa na wazawa? Wazawa kushusha bei kama mchina? au kumfukuza mchina?
 
Na huku Tanzania, hili linaweza kuwa ni jambo la muda tu. Mchina hana papara. Mchina ameanza kupunguza watu wanaopata vibali vya kwenda China, kaweka warehouse zake happ Ubungo, na hatua kwa hatua anaendelea kusukuma kete zake kwa umakini.

Ukweli ni kwamba, kadri muda unavyoenda, Wachina watazidi kujaa kwenye biashara. Serikali inaweza kuwa inatoa matumaini hasa kipindi cha uchaguzi, lakini Mchina naye si mtu wa kukurupuka. Anafanya hesabu zake za muda mrefu, akitumia mikopo na misaada kujenga mazingira yatakayomruhusu kufungua soko lake huku kwetu.

Na ukweli mwingine mchungu ni kwamba serikali haiwezi kubadilisha sera zake kwa sababu tu wafanyabiashara hawafurahishwi na ushindani wakati huo washapewa misaada kibao na kuna mikopo wanadaiwa.

Hata mkisema Wachina waondoke sokoni na waende kufanya biashara sehemu nyingine, watu bado watawafuata huko waliko. Kwa hiyo, suluhisho si kuwafukuza Wachina sokoni au kuwahamisha kutoka eneo moja kwenda jingine. hilo ni suluhisho la muda mfupi tu, sio permanent.

Ni aidha wafanyabiashara wabadilike au wasubiri anguko

Biashara inabadilika, na dunia inabadilika. Hakuna biashara inayobaki vilevile milele. Kama ushindani umeongezeka, wafanyabiashara nao wanapaswa kubadilika.

Kukimbizana na Mchina kila anapoenda hakutamaliza tatizo. Mchina anayekutengenezea karibu kila kitu unachonunua ni vigumu kushindana naye kwa kuuza bidhaa zilezile tu.

Cha muhimu ni kujua namna ya kuishi na ushindani mpya. Biashara ya zamani inaweza kufa, lakini mfanyabiashara anayebadilika anaendelea kuishi.
 
Uwiano utaletwa kwa mchina kuuza bei kubwa sawa na wazawa? Wazawa kushusha bei kama mchina? au kumfukuza mchina?
Una majibu ya harakaharaka na unatoa hitimisho bila ya kuzama kwenye mada!
... unafahamu wachina wanachofanya? Sio muda mrefu watachukua uchumi wote wa biashara na ndipo unyonyaji wao utakapojidhihirisha!
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Back
Top Bottom