Kwa ufupi...huu mgogoro unapata trace kwenye Darfur War..2003 huko.
Mnakumbuka kipindi kile palikuwa na wale jamaa wanaitwa Janjaweed-Kikundi cha kipigani upande wa serikali lkn nje ya jeshi..kilichoundwa na waafrika waliojifanya waarabu pamoja na waarabu wenyewe..Kikundi hiki ndio kilikuwa ingine ya Omari Ally Bashiri..
Baada ya vita kikabadirishwa jina na kuwa Rapid Support Force...lkn kikakataa kuingizwa kwenye mfumo rasmi ya jeshi. Kikundi hiki kilishirikiana na jeshi kumpindua Omar 2019 (Ingawa pia hawa ni kama wapo upande wa Bashiri hadi leo).
Baada ya Bashiri kupinduliwa kikundi hiki kimekataa maridhiano ya kujiingiza kama moja ya vikosi vya serikali..sababu kinaogopwa kitapotez influence na nguvu, pili hawa jamaa RSF wanalipwa mishahara na Wizara ya Fedha moja kwa moja sio kupitia wizara ya Ulinzi, hivyo kuingizwa huko watapoteza hizo favours.
Pia mkuu wa hiki kikundi na mkuu wa jeshi rasmi...wanautofauti wa nani atapaswa kuwa mkuu wa majeshi..kama kitaingia kama kitakuwa sehemu ya Jeshi.
Pia hiki kikundi- hakitaki utawala wa kiraia 100%..Wanataka jeshi libaki na nguvu na say..kama ilivyo sasa na ilivyokuwa baada ya mapinduzi..
Ukiangalia hapo, ugomvi huu chanzo ni:
Pesa, madaraka, ushawishi, wizi..
Kunataarifa kuwa kimetumika na mataifa ya Ulaya..ili kuzuia Jeshi kuwapatia Urusi sehemu ya kujenga base...