Wanajeshi (JWTZ) Wasaidie kufundisha maadili na Uzalendo Majeshi mengine ya Tanzania

Jwtz wanajiheshimu na hawana maujinga kama majeshi mengine na wao wamenyooka straight forward na hawataki utani. Mimi mtu akiniambia eti uhamiaji, police ni jeshi nakataa maana wao ndio wahalifu number one wanaokula rushwa na uchafuzi mwengine
Uhamiaji ni Idara, polisi ni jeshi lakini pia kufananisha hizi Taasisi na kumtafuta Superior ni upuuzi kuliko Rushwa yenyewe.
Kila Taasisi ina weledi katika majukumu yake na ina udhaifu pia katika majukumu yake

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
 
Uhamiaji ni Idara, polisi ni jeshi lakini pia kufananisha hizi Taasisi na kumtafuta Superior ni upuuzi kuliko Rushwa yenyewe.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
Uhamiaji imeshakuwa jeshi Sasa hivi, kamili na hao police ndio wahalifu wenyewe na hapa hatulinganishi ila tunaangalia uadilifu kitu ambacho kiko jeshini pekee
 
Maadili na uzalendo ni ideology ambayo haipandikizwi kwa miezi mitatu ya kua jkt.

Skendo ngapi ziliibuka kipindi cha Kikwete ambacho ndicho kilipeleka viongozi jkt? Nafikiri kuna viongozi walihusika kwenye skendo na walikua wameenda jkt.

Na kuna viongozi walipita jeshini ila chini ya utawala wao rushwa na ubadhirifu vilikithiri.
 
Uhamiaji imeshakuwa jeshi Sasa hivi, kamili na hao police ndio wahalifu wenyewe na hapa hatulinganishi ila tunaangalia uadilifu kitu ambacho kiko jeshini pekee
Uhamiaji bado ni Idara, pia hapo ulipo katika kutekeleza majukumu yako lazima muwe na itikadi tofauti za kitabia na kimaadili japo mnasimamia muongozo mmoja.

Sent from my iphone using JamiiForums mobile app
 
JWTZ ni Jeshi letu bora kabisa la kujivunia, kama ilivyo vyombo vyetu vyote vingine vya ulinzi na usalama. Ukijenga hoja kuhusu taasisi usipende fallacy generalization. Hizo taasisi nyingine ulizozitaja kirahisi zina kazi kubwa mno kwa ajili ya usalama wa nchi na raia. Kosoa tuhuma za maadili za mtu siyo taasisi maana taasisi haiwezi kupanga uovu.

Kwa mfano, mtu hawezi kusema JF yote ni ya hovyo kwa sababu tu ya watu wachache wenye hoja jumla kama hii ya kwako.
 
Hakuna uzalendo pasipo kuwa na haki na hakuna uzalendo pasipo kuwa na usawa

Mfano: familia ya mbowe inaweza kuwa na uzalendo na Tanzania?,, Familia ya lissu inaweza kuwa na uzalendo na Tanzania,

Utafutwe usawa na haki kwanza ndipo uzalendo utakuja wenyewe sio kutaka uzalendo KWA mtu unaye mpiga makofi behind the scenes
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…