Wanajeshi Mali wauawa siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kuondoa vikosi vyake

Wanajeshi Mali wauawa siku chache baada ya Ufaransa kutangaza kuondoa vikosi vyake

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mali.jpg

Jeshi nchini Mali limesema wanajeshi wake wanane wameuawa na watano hawajulikani walipo baada ya kushambuliwa na waasi katika eneo la Kaskazini-Mashariki la Archam.

Mapigano hayo yanakuja siku chache baada ya Ufaransa na washirika wake kusema kuwa wanaondoa vikosi vyao kutoka Mali.

Taarifa ya jeshi ilisema kuwa katika kukabiliana na shambulio hili la hivi punde zaidi, jeshi la anga la Mali liliwaua wanamgambo 57.

Ilisema kuwa wanajeshi hao walikuwa wakitafuta maficho ya waasi walipoviziwa na "watu wasiojulikana wenye silaha".

Kumekuwa na wasiwasi wa kieneo na kimataifa kuhusu usalama wa Mali kufuatia kutimuliwa kwa wanajeshi wa Ufaransa, pamoja na uthibiti wa mamluki wa Urusi katika eneo hilo.

Wiki hii pekee, wenyeji waliliambia Shirika la Habari la AFP kwamba raia 40 wameuawa katika eneo moja la Archam ambako makundi hasimu ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Islamic State, yanaendesha harakati zake.

Mali imekuwa ikikabiliana na machafuko ya wanajihadi kwa miaka mingi, na kusababisha maandamano makubwa mwaka 2020 dhidi ya Rais wa wakati huo Ibrahim Boubacar Keïta ambaye aliondolewa madarakani na viongozi wa mapinduzi wakiahidi kurejesha usalama.

Tangu wakati huo viongozi wapya wa kijeshi wa nchi hiyo wamekuwa na msururu wa kutoelewana na mkoloni wa zamani, Ufaransa, hali iliyowafanya kukataa makubaliano ya kufanya uchaguzi wa kidemokrasia mwaka huu na kumfukuza balozi wa Ufaransa alipopinga.

Ilifikia kilele kwa Mali kuamuru Ufaransa kuondoa wanajeshi wake wote, baada ya karibu miaka 10 kupambana na tishio la wanajihadi.

Wakiungwa mkono na wanajeshi kutoka mataifa mengine ya Magharibi, ujumbe wa pamoja wa Mali - unaoitwa Kikosi Kazi cha Takuba - sasa utahamia umbali mfupi kuvuka mpaka hadi Niger, ukisalia karibu na kambi yao ya sasa.

Rais wa Niger alisema siku ya Ijumaa kwamba mipaka ya nchi hiyo huenda ikawa hatarini zaidi kwa shughuli za wanamgambo wa kijihadi kufuatia kuondoka kwa vikosi vya Ufaransa na washirika wao kutoka Mali.

Mapema wiki hii yeye na viongozi wengine wa Afrika Magharibi walikutana na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kabla ya tangazo la kuondolewa kwa vikosi kutoka Mali, ambapo walikubaliana kuwa wanajeshi hao watahamia nchi za eneo hilo.
 
Pole yao sana...

Sisi huku magaidi wanakutwa na shangazi kaja...
 
Back
Top Bottom