gallow bird
JF-Expert Member
- Aug 10, 2024
- 14,889
- 18,593
Mamlaka za Ubelgiji zimesema ziliwakamata na kuwahoji kwa muda mfupi raia wawili wa Israel waliokuwepo kwenye tamasha la muziki la Tomorrowland wiki iliyopita, baada ya makundi yanayoiunga mkono Palestina kuwatuhumu kwa makosa ya kivita.
Mwendesha mashtaka alisema walipokea malalamiko kwamba askari wawili wa Israel walioshiriki vita huko Gaza na kukiuka sheria za kimataifa walionekana kwenye tamasha hilo lililofanyika karibu na mji wa Antwerp.
Polisi waliagizwa kuwatafuta na kuwahoji, kisha wakaachiliwa baada ya mahojiano. Mamlaka zilisema zina mamlaka ya kushughulikia makosa ya kivita hata kama yalifanyika nje ya nchi yao. Hawakutoa maelezo zaidi kuhusu uchunguzi huo.
Majina ya Waisraeli hao hayajatajwa.
Shirika la Hind Rajab Foundation, linalotetea Wapalestina, linasema lilitambua askari wawili wa Israel waliowajibika na mauaji huko Gaza kati ya watu waliokuwa kwenye tamasha. Walisema baadhi ya vijana kutoka Israel walionekana wakipeperusha bendera ya kikosi cha kijeshi cha Givati, ambacho kimeshiriki mapigano Palestina.
Shirika hilo liliwasilisha malalamiko kwa kushirikiana na kikundi cha wanasheria cha Global Legal Action Network kinachopigania haki za binadamu.
Tomorrowland ni moja ya matamasha makubwa zaidi ya muziki wa elektroniki duniani, likihudhuriwa na maelfu ya watu kutoka sehemu mbalimbali. Mwaka huu, watu wapatao 400,000 wanatarajiwa kuhudhuria kwa awamu mbili tofauti.
==========================
Belgian authorities have said they briefly held and questioned two Israeli citizens who attended an electronic music festival last week, after pro-Palestinian groups accused them of war crimes.
Prosecutors said they had received legal complaints alleging that two Israeli soldiers responsible for “serious violations of international humanitarian law” in Gaza were spotted at the Tomorrowland festival near the northern city of Antwerp.
The federal prosecutor’s office said it had asked the police to locate the two people named in the complaint and to interview them. “Following these interviews, they were released,” it said in a statement.
The office said it had taken action after concluding that Belgian courts had extraterritorial jurisdiction over alleged war crimes. “No further information will be given at this stage of the investigation,” the office said.
The two Israelis have not been named.
Source: The Guardian