POTOSHI Wanajeshi wa Iran waachia video namna walimvyomkamata rubani wa Marekani

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Wakuu

Je, hii video ni ya hivi karibuni?



Your browser is not able to display this video.
 
Tunachokijua
Kupitia mitandao ya Kijamii kumekuwapo na video inayosambazwa na watumiai wa kawaida wa mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari na kudai kuwa ni video iliyoachiwa na jeshi la Iran wakimkamata rubani wa Marekani. Video hiyo inajiri baada ya April 03, 2026 Iran kueleza kuwa ndege ya Marekani ilitunguliwa nchini humo.

Chombo kimoja cha habari kilichapisha video yenye grafiki na ujumbe unaosomeka;

IRAN WAACHA VIDEO WALIVYOMKAMATA RUBANI WA MAREKANI


Uhalisia wa video hiyo: POTOSHI

Ufuatiliaji uliofanywa kwa kutumia nyenzo za kidigitali umebaini kuwa video hiyo haihusiani n amgogoro unaoendelea kati ya Iran, Israel na Marekani kama ilivyodaiwa.

Kwa kutumia Google reverse image search imebainika kuwa video hiyo imekuwepo mtandaoni kuanzia Machi 02, 2026 na walioichapisha walieleza kuwa ni tukio lililotokea nchini Libya.

Chombo kimoja cha habari kutoka nchini Libya kinachofahamika kwa jina la Fawasel Media kilichapisha video hiyo Machi 02, 2026 na kuambatanisha ujumbe unaosomeka:

"Tazama | Mfanyakazi wa Kikosi cha Lightning kutoka Benghazi akiruka kwa parachuti licha ya kuwa na mfupa uliovunjika mguuni, huku wenzake wanamkaribisha baada ya kutua. #Libya"


Mtumiaji mwingine kuitia ukurasa wake wa Instagram alichapisha video hiyo hiyo tena Machi 02, 2026 kuelezea tukio hilo la Wanajeshi wa Libya. Aliandika:

"Mandhari ya uthabiti wa hali ya juu—aliruka kwa ujasiri licha ya kuwa amejeruhiwa kwa kuvunjika mguu. Hivyo, wanajeshi wetu ni mashujaa wa Jeshi la Kiarabu la Libya. Alhamdulillah, ametua salama."


Your browser is not able to display this video.


​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…