Wanajeshi wa Urusi waliiambia BBC: 'Tulishuhudia wenzetu wakiuawa kwa amri ya makamanda wetu'

Wakusoma 12

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Posts
5,503
Reaction score
15,858
Dima anasema alishuhudia askari mwenzake akiuawa kwa amri ya moja kwa moja ya kamanda wake. Dima anasema alishuhudia askari mwenzake akiuawa kwa amri ya moja kwa moja ya kamanda wake.
Maelezo kuhusu taarifa

Onyo: Taarifa hii ina maelezo ya vurugu iliyokithiri na marejeleo ya kujiua.

Wanajeshi wanne wa Urusi wameeleza kwa kina hali ya ukatili na mateso waliyoishuhudia katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine. Wawili kati yao walithibitishia BBC kuwa waliona wanajeshi wakipigwa risasi na kuuawa papo hapo kwa sababu ya kukataa kutekeleza amri za kijeshi.

Mmoja wao aliiambia timu ya watayarishaji wa makala ya BBC kwamba alimwona mwanajeshi akiuawa kwa amri ya kamanda wake, kamanda ambaye baadaye alitunukiwa cheo cha "Shujaa wa Urusi" mwaka 2024.

Mwanajeshi mwingine kutoka kikosi tofauti alieleza kuwa alimwona kamanda wake akiwapiga risasi watu wanne kwa mikono yake mwenyewe.

"Niliwajua," alisema. "Nakumbuka mmoja wao akipaza sauti: 'Usinipige risasi, nitafanya chochote utakachosema!'"

Mtu mwingine alisimulia kuwa aliona miili ya wanajeshi wenzake ishirini ikiwa imetupwa kwenye shimo baada ya "kuondolewa", neno la msimu wa kijeshi wa Urusi linalomaanisha kumuua mwanajeshi mwenzako.

Katika makala ya televisheni Zero Line: Inside the Russian War, wanaume hao wanasimulia kwa maelezo ya kutisha jinsi walivyoteswa kwa kukataa kushiriki mashambulizi waliyoyafananisha na operesheni za kujiua.

Jeshi la Urusi hurejelea mashambulizi hayo kama "meat storms", yaani, mawimbi ya wanajeshi yanayotumwa kuvuka mstari wa mbele bila kukoma kwa lengo la kuichosha na kuipunguza nguvu adui.
 
Katika mahojiano hayo ya BBC,
aliethibitisha kwamba hao wanajeshi ni wa Urusi ni nani?

Jeshini tena mstari wa mbele katika uwanja wa vita sio mahali pa kuleta drama otherwise utakua eliminated tu ili kupave the way kwa waliotayari kusonga mbele bila kukatishwa tamaa au kutatizwa na uoga wa mamaluki moja au wawili tu kikosini.

Hakuna jeshi duniani linaloweza kumvumilia askari anae resist amri ya kijeshi vitani, kwani ikiwa yupo basi huyo ni aduni namba moja anafaa kua eliminated mara moja.
 
Dima anasema alishuhudia askari mwenzake akiuawa kwa amri ya moja kwa moja ya kamanda wake. Dima anasema alishuhudia askari mwenzake akiuawa kwa amri ya moja kwa moja ya kamanda wake.
Maelezo kuhusu taarifa

Onyo: Taarifa hii ina maelezo ya vurugu iliyokithiri na marejeleo ya kujiua.

Wanajeshi wanne wa Urusi wameeleza kwa kina hali ya ukatili na mateso waliyoishuhudia katika mstari wa mbele wa vita nchini Ukraine. Wawili kati yao walithibitishia BBC kuwa waliona wanajeshi wakipigwa risasi na kuuawa papo hapo kwa sababu ya kukataa kutekeleza amri za kijeshi.

Mmoja wao aliiambia timu ya watayarishaji wa makala ya BBC kwamba alimwona mwanajeshi akiuawa kwa amri ya kamanda wake, kamanda ambaye baadaye alitunukiwa cheo cha "Shujaa wa Urusi" mwaka 2024.

Mwanajeshi mwingine kutoka kikosi tofauti alieleza kuwa alimwona kamanda wake akiwapiga risasi watu wanne kwa mikono yake mwenyewe.

"Niliwajua," alisema. "Nakumbuka mmoja wao akipaza sauti: 'Usinipige risasi, nitafanya chochote utakachosema!'"

Mtu mwingine alisimulia kuwa aliona miili ya wanajeshi wenzake ishirini ikiwa imetupwa kwenye shimo baada ya "kuondolewa", neno la msimu wa kijeshi wa Urusi linalomaanisha kumuua mwanajeshi mwenzako.

Katika makala ya televisheni Zero Line: Inside the Russian War, wanaume hao wanasimulia kwa maelezo ya kutisha jinsi walivyoteswa kwa kukataa kushiriki mashambulizi waliyoyafananisha na operesheni za kujiua.

Jeshi la Urusi hurejelea mashambulizi hayo kama "meat storms", yaani, mawimbi ya wanajeshi yanayotumwa kuvuka mstari wa mbele bila kukoma kwa lengo la kuichosha na kuipunguza nguvu adui.
Supa-pawa Urusi hana masihara
 
Back
Top Bottom