Wanajeshi walazimisha Raia kujenga Daraja

Wanajeshi walazimisha Raia kujenga Daraja

Kichakoro

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2008
Posts
3,335
Reaction score
6,186
Daraja la Mpiji Kidimu ambalo limefadhiliwa na JWTZ ni la msaada Sana kwa wakazi wa eneo Hilo.

Kumekuwa na ukarabati wa Daraja Hilo kwa zaidi ya Mwezi mmoja Sasa. Ila tangu wiki iliyopita wanajeshi wanaojenga Daraja Hilo wamekuwa wakiwalazimisha wakazi wapitao darajani hapo kufanya shughuli za ujenzi kwa lazima.

Kila anayepita hulazimishwa kubeba mawe au kazi ingine waifanyayo walau kwa nusu saa.

Hii ni kinyume na utaratibu maana Kama inahitajika nguvukazi Mtendaji kata/Kijiji/mtaa husika alipaswa kuwaambia wananchi kuhusu kujitolea huko badala yake wanajeshi wameamua kujifanyia watakavyo.

Pili wao wanalipwa na jeshi pamoja na Tanroad/Tarura kuifanya kazi hiyo. Hivyo kuwalazimisha raia kuifanya ni kinyume na taratibu.

Tunaomba jeshi kufanya uchunguzi na kuchukua hatua haraka maana umesababisha usumbufu mkubwa na kufanya watu kuzunguka umbaki mrefu kuwakwepa, kuvuka mto maeneo ambayo sio salama.

Daraja lipo mpiji Magoe chama Kama unaenda kibamba ulizia Daraja la jeshi. Mamlaka husika zichukua hatua kunusuru Hali kabla ya kusababisha madhara kwa raia
 
Jana nilitaka kupita barabara hiyo kutokea Baobab njiapanda ya Vikawe ndio nikaambiwa kuna ujenzi wa Daraja unaendelea mbele, nikabadili uelekeo na kuendelea mbele njia ya wazo hill.
 
Back
Top Bottom