Wanajeshi wetu wanajisikiaje??

Raia mpya

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2022
Posts
673
Reaction score
1,915
Salaam ndugu zangu kuna jambo limenifikirisha kidogo baada ya juzi kuja huyo mgeni kutoka Usa sasa baada ya kutua tu kila kitu cha ulinzi kilikuwa chini ya wageni kuanzia Airport mpka sehemu alipokuwa huyo mgeni na mpaka anaondoka wanajeshi wa kigeni ndio walikuwa wanaosimamia show nzima ya ulinzi ya viongozi wote wawili,
Sasa najiuliza hivi wanajeshi wetu wanajisikia kuona nchi yao inalinda na wengine ina maana wao hawaaminiki??
 
Hiyo ni kawaida, na mifumo yote ya Serikali inajuwa. Siyo mara ya kwanza hilo kutokea kwani hata George Bush Jr, na Barack Obama walipokuja security protocol ilibadilika. Mind you USA ndiyo dunia
 
Wacha waendelee kujifunza.
 
Marekani taifa kubwa mno hivyo hakuna tatizo wao kujisimamia kiulinzi.
 
Wanajeshi wanalinda mipaka ya nchi, labda swali lako lingeenda kwa Polisi na vyombo vingine vya ulinzi wa ndani
 
Wakati wa JK walipanda hadi darini kule jumba jeupe
 
Washazoea siyo mara Yao ya Kwanza kufanywa hivyo
 
Sasa kama hatuko compentence kwa medani za kijeshi inabidi washike wao tu ili likitokea la kutokea wa kulaumiwa ni wao. Hawa jamaa huwa wanajiona ni superior zaidi kuliko majeshi yote duniani. Wanafanya hivyo kwa nchi zenye uwezo mdogo wa kijeshi. Wakienda uingereza, china na urusi hawawezi kuweka pembeni majeshi ya nchi hizn washike wao. Hawana imani na ulinzi wa majeshi ya nchi masikini na huwa kero kwa kiongozi wao anapotembelea nchi hizo
 
Wanajeshi wetu hawana uwezo kama wanajeshi wa USA.

Ni jambo la Busara kukaa pembeni kama walivyofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…