Ghaddaf naye alianza kuiga ushenzi huo anapotembelea nchi za waafrika wenzake anawapa kero na yale mahema yake ya kibedui. Eti naye alijionesha ana ulinzi imara kuliko wa nchi mwenyeji wake. Cha ajabu aliuwawa kama paka mwizi pasipo na huo ulinzi, tena kifo cha kutia huruma kana kwamba hakuwahi kumiliki majeshi na vikosi imara nchini mwake. Hawa wamerekani wana dharau na kiburi kwa vyombo vya ulinzi na usalama vya nchi zetu, hawajakutana na rais wa nchi asiyependa dharau kwa majeshi yake ya ulinzi, hao wanajeshi wao watawekwa kando watulie nchi mwenyeji isimamie shoo nzima ya ulinzi na usalama. Rais wao akiwa anatua na yale madege yao air force wanakuwa na wasiwasi hata na vitu visivyo hai wanavikazia macho kana kwamba ni hatari. Wanapenda kufunuafunua lile zulia jekundu mpaka wanakera. Wakiona kikaratasi kidogo kinapeperushwa na upepo wanakitolea macho na kukikaribia kujua ni kitu gani. Kama tumewakaribisha nyumbani kwetu watuamini mwanzo hadi mwisho hata sisi tunajua ulinzi na usalama kama wao, tuheshimiane