WanaJF mnakumbuka hii hadithi? Sadiki na Chitemo

WanaJF mnakumbuka hii hadithi? Sadiki na Chitemo

Tukumbushie Manenge na Mandawa
21909468_1541814489195701_4981986072780079104_n.jpg
 
SADIKI NA CHITEMO




Sadiki ni mtoto anayeishi karibu na Ujiji. Anaye ndugu yake aitwaye Sikiri. Sadiki na Sikiri husoma katika shule ya Businde. Sadiki anafanya kazi zote kwa bidii. Lakini Sikiri ni mtoto mbaya kwa sababu ni mvivu, kaidi, tena hana adabu.
Siku moja wakati wa livu baba yao aliwaamsha mapema sana. Akasema, "Sadiki, chuukua hii shilingi. Nenda sokoni ukanunue samaki. Na wewe Sikiri, nenda kisimani ukateke maji." Wote wawili wakaenda. Sadiki alinunua samaki, akarudi nyumbani haraka. Lakini Sikiri alichelewa. Baba yake akamngoja mpaka akachoka.
Baba akatoka kwa hasira kumfuata Sikiri kule kisimani. Alipofika alimkuta anachezea maji. Anayateka na kuyamwaga juu ya jiwe. Baba yake akamwuliza, "Unafanya nini Sikiri? Mbona unacheza tu? Teka maji, twende nyumbani." Sikiri akateka maji, wakarudi nyumbani.
Walipofika nyumbani walimkuta mama amekwisha tayarisha uji. Wakanywa. Walipomaliza, baba yao akawaambia, "Twendeni tukapalilie bustani ya mboga. Mama atabaki hapa nyumbani. Atalisha kuku na kusafisha nyumba. Baadaye atatayarisha chakula."
Kule katika bustani kulipandwa mchicha, maharagwe, vitunguu na nyanya. Magugu na manyasi yaliota kwa wingi. Sadiki, Sikiri na baba yao walipalilia kwa uangalifu ili wasiharibu mimea ya mazao.
Sikiri hakupenda kazi. Kwa hiyo alitoroka akaenda kichakani. Kule kichakani alitafuta matunda mwitu. Sikiri alikuwa mtoto mvivu kweli. Hakutaka kufanya kazi kwa bidii. Sadiki na baba yake waliporudi nyumbani, akawafuata.
Walipofika nyumbani chakula kilikuwa tayari. Sikiri alikuwa wa kwanza kunawa mikono na kuanza kula. Siku ile mama alipika ugali na samaki alionunua Sadiki. Walipokwisha kula, baba alimwita Sikiri akamwuliza, "kwa nini leo alitoroka?" Sikiri alinyamaza tu. Sakiri alikuwa mtoto mkaidi. Baba akamwambia, "Kesho utakwenda kupalilia bustani. Usipokwenda hutapata chakula."
Siku iliyofuata Sikiri alikataa kwenda bustanini, alitoroka. Sadiki na baba yake walikwenda kupalilia peke yao. Jioni waliporudi, baba alimwuliza mama, "Sikiri amekwenda wapi?" Mama akajibu, "Mimi leo sijamwona nyumbani. Sijui amekwenda wapi." Kumbe, siku ile asubuhi Sikiri alipanda basi kwenda mjini Kigoma. Huko njiani aliulizawa nauli. Sikiri hakuwa na pesa hata kidogo. Dereva akamtelemsha pale pale. Akaachwa peke yake. Sikiri alilia sana . Mwisho akaanza kusema kwa uchungu:-
Sikiri mimi maskini,
Uvivu wangu nyumbani,
Ukiwa huu njiani,
Nakufa hapa kwa nini?

Sadiki sasa ashiba,
Chakula kingi kwa baba,
Nirudi tena kwa baba,
Nakufa hapa kwa nini?
Sikiri alirudi nyumbani. Alikuwa amechoka sana. Alipofika nyumbani aliomba radhi. akamwambia baba na mama.
Naomba radhi nimekosa,
Nitakuwa mtoto mwema sasa,
Shambani tena sitakosa,
Baba na mama nisameheni.

Nitalima kama Sadiki,
Nitalima wala sichoki,
Na nyumbani tena sitoki
Baba na mama nisameheni.
Baba hakumpiga Sikiri. Alimsamehe. Sikiri akabadili tabia yake, akawa anawasaidia wazee wake. Kila alipotumwa alikwenda upesi. Mama yake alifurahi, akamwambia, "Siku hizi wewe ni mtoto mwema kama Sadiki. Mtoto mtii hupendwa na wazazi wake. Tena hupendwa na watu wote kijijini. Endelea kuwa mtoto mwema na mtii.......MWISHO......
Nimeisoma mwaka 94 ..kipindi hicho ilikuwa ni sadiki na sikiri
 
Yaani kwa kuthibitisha kuwa "...hatuna utamaduni wa kutunza elimu", hivi vitabu havipatikani kabisa. Kuna siku nimeingia maktaba ya Mkoa, nikaulizia kama naweza pata nakala ya vitabu vya shule ya msingi vya zamani, nikajibiwa hakuna, yaani nikabaki najiuliza "nina kosa gani mimi ambaye sikuvitunza"
 
Back
Top Bottom