Kweli wewe ni Al-Watan![emoji4]Nimefurahia kiswahili fasaha ulichokianda hapa. Natamani watangazaji wa runinga, wabunge, viongozi mbalimbali wangeongea Kiswahili kilichonyooka sio kuchanganya lugha mbili wakati wanajua fika kwamba raia wengi Kiswahili ndio wanachokielewa zaidi. Man! I think the last time I used these two words "sarufi" & "istilahi" was in primary & secondary school, that was a while ago. Naamini tunao uwezo wa kusoma masomo yote hadi elimu ya juu kwa lugha yetu wenyewe, ni muhimu kutupilia mbali minyororo ya kung'ang'ania lugha za watu. Wachina, Wajapani, Waethiopia, Waarabu, Wahindi na mataifa kibao duniani wanajivunia kutumia lugha zao na wanasonga mbele. Sisi hapa bado tunachekana eti fulani hajui Kiingereza, ni ulimbukeni, kwa mawazo yangu.