WanaJF naomba kukumbushwa; zawadi nono kupitia M-PESA, Tigo Pesa, au Airtel Money kwa atakae patia

Pi Network

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2016
Posts
290
Reaction score
319
Jamani kuna kitu nilikuwa natazamia kukifanya mda mfupi ujao, lakini kitendo tu kuingia humu ndani na kukutana na habari moto moto nyingine zenye kuburudisha, nyingine za kusisimua, na nyingine zenye kuhuzunisha kimesababisha kusahau hata nilichokuwa natarajia kufanya.

Hivyo kama kichwa cha habari kinavyojieleza shilingi 50,000/= itatolewa kwa atakae patia.

Nitakuwa mwaminifu kwa atakae shinda, na nakala ya malipo nitaiweka hapa hapa kwa idhini ya mshindi.

NB:
Vigezo na masharti kuzingatiwa.


[UPDATE ] Mshindi wa bahati nasibu hii atatangazwa kesho asubuhi kupitia thread hii; hivyo washiriki wote na wanaoendelea kushiriki mnashauriwa kushiriki zaidi na zaidi kadili mtu awezavyo. Lakini pia hapo kesho mda wa saa mbili asubuhi jina la mshindi litabandikwa hapa na pesa yake itatumwa kwa njia ya simu ya mkononi kisha nakala ya malipo itawekwa hapa kama ushahidi.

Wenu mwaminifu "Wamjengoni"
 
Ulitaka kuingia FACEBOOK😡😡😡
 
Kitu ulichokua unataka kukifanya ni KUINGIA NDANI'
 
Ulikuwa unataka kwenda kumsalimia ndugu
 
Ulikuwa unataka kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi huko Kagera.
 
Ulikuwa unataka kuchangia waathirika wa tetemeko la ardhi huko Kagera.
Dah! Yaani we ndo unazidi kunichanganya kabisa yaani, naijutia hela yangu niliyochanga kwa ajili yao [emoji17]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…