WanaJF waliohesabiwa na wale ambao hawajahesabiwa, mapumziko ya leo yamewasaidiaje?

WanaJF waliohesabiwa na wale ambao hawajahesabiwa, mapumziko ya leo yamewasaidiaje?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kwa kuwa kujifunza hakuna kikomo, natamani kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko yanayofanywa katika nchi yetu hasa kwa awamu hiiya sasa!

Kwa kuwa kujifunza hakuna kikomo, natamani kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko yanayofanywa katika nchi yetu hasa kwa awamu hiiya sasa!
Kazi rahisi lakini wameipromoti kwa nguvu za ajabu
 
Kwa kuwa kujifunza hakuna kikomo, natamani kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko yanayofanywa katika nchi yetu hasa kwa awamu hiiya sasa!
Kwa kuwa "kujifunza hakuna mwisho", binafsi nilichojifunza harakaharaka kutokana na sensa hii ni hiki.

Ghrama za zoezi zima linasemekana kuwa $141 milioni (pesa ya kimarekani).

Tumekopa, au tumepewa msaada kwa kiasi kikubwa kwenye gharama hizi. Hii ni baada ya miaka 60 tokea tulipojitangazia kwamba tunataka kuwa huru, tufanye mambo yetu kwa uhuru wetu wenyewe.

Binafsi ningependa kujuwa mambo ambayo tunaweza kuyafanya sisi wenyewe bila ya kumtegemea mfadhiri yeyote.
Hapo nitakuwa nimepanua upeo wangu katika mambo ambayo nilikuwa siyafahamu.

Kuhusu "mabadiliko yanayofanywa katika nchi yetu...); nadhani yapo mabadiliko mengi sana kwa sasa. Nielewe vizuri. Mabadiliko siyo lazima yawe chanya, ndipo yaonekane kuwa ni mabadiliko.

Zoezi lenyewe la sensa linavyoonekana na kuendeshwa, ni mabadiliko yasiyotia matumaini sana juu ya hatima ya nchi hii. Ni kama mzaha mzaha tu!
 
Huku niliko mtaa mzima hakuna aliye hesabiwa! Tunasubiri tuone kuanzia kesho na hizo siku 6 zilizobaki kama watapitia kutuhesabu..
 
Kwa kuwa kujifunza hakuna kikomo, natamani kujifunza zaidi kuhusu mabadiliko yanayofanywa katika nchi yetu hasa kwa awamu hiiya sasa!
Nimehesabiwa leo 🖐️
 
...
IMG-20220823-WA0029.jpg
 
Tatizo hii nchi imejaa upigaji tu... Kila apataye nafasi anawaza apigeje... Ndio maana mambo hayafanyiki yanavyotakikana..... Ilipaswa kabla kila mjumbe apewe vipeperushi vya maswali yatakayoulizwa agawe kwa watu wake. Mjumbe angechagua na kuzitaarifu nyumba ambazo zitahesabiwa siku husika ili wengine waendelee na shughuli zao. Na mtu kama ana udhuru taarifa amwachie mjumbe maana tayari anayajua maswali.
 
Back
Top Bottom