Wanajua kuimba ila jeuri na kiburi vina warudisha nyuma

pwilo

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
10,913
Reaction score
13,876
1. Ali kiba

Moja kati ya wasanii ambao wamejaaliwa kipaji na sauti nzuri ila jamaa anajiamini kupita kiasi na ili akubali ushauri au idea ya kuendeleza kipaji chake nguvu kubwa sana inahitajika. Kilichotokea kati yake na Davido pamoja na MI wa aje ni ushahidi wa ninachokiongea na hata aliye mshauri idea ya team samatta na team kiba alifanya kazi kubwa sana mpaka akakubali wazo hilo.

2. Ruby

Mwanadada mwenye sauti murua ya kumtoa nyoka pangoni hakusita kuwagomea ma boss wake kwa kudai pesa aliyokuwa amepewa ni kidogo hivyo hatashiriki kwenye tamasha lao na kuingia katika mgogoro mkubwa ulio isha siku za karibuni.

3.Barak da prince

Moja kati ya wasanii ambao walikuja vizuri sana kipindi cha mwanzoni na kufanya vizuri na nyimbo yake ya SIACHANI NAWE na baada ya hapo ni ngoma Kali mfululizo ila jamaa ni jeuri sana kitu kinacho fanya baadhi ya media kumpotezea.

4.Timbulo

Kinacho muangusha huyu jamaa kwanza sio mtu wa kujichanganya sana anaishi maisha tofauti na wasanii wenzake baada ya kugombana na media ambayo bila wao kimziki huwezi kutoboa kutokana na maslahi yake na wakaamua kumpotezea.

5. Young killer (msodoki)

Huyu jamaa tatizo lake anajisifia sana
Na kuwadharau baadhi ya wasanii wenzake wakiwemo wakongwe (weusi) na kudai kuwa kuna baadhi Yao wana bebwa na media ila hawana uwezo wowote kulinganisha na yeye kama janjaro na young Dee hivyo kufanya baadhi ya media na wasanii wenzake kumpotezea.

Wapo wengi ila hao ni wachache tu kati Yao kama wakiacha hizo Tabia walizo nazo na kuweka juhudi kwenye mziki wao wangefika mbali sana ila ndo hivyo kipato huleta majivuno.
 
Hapo kwa killer. Kwahiyo ukigombana na weus na hao Dogo janja sijui na young d ndo unakuwa na kibul? Na media zina acha kucheza kaz zako

Nani kwanza kakwambia young killer kapotea au kwa sababu humuon kwenye hilo tamasha Wa wendawazim
 
young killer ukitizama kwa makini graph yake...utagundua inashuka kwa kasukichukua dear gambe na umebadilika...utajua young killer wa leo ni kelele tu.
kilichompata nikki mbishi ndio kinachoenda kumpata young killer....hawa wote wanasifa moja ya kujiona wanajua sana kiasi kwamba wanabadili na style zilizowatoa
 
Ww jamaa upo long time kitambo sana sijakuona jukwaani Yoooooh
 
Hao wasanii uliwataka nn wakakujeuria? Maana mtaani bado kuna Joto la KONKI KONKI KONKI MASTER na mambo ya Mitaro!
 
Napenda mziki wa young killer anajua lakin saiv simuelewi kabisa sijui ni sifa zimezid ila ameporomoka sio kama mwanzo saiv anaimba hip hop taarab mipasho
 
kama hujikubali naani mwingine akukubali boss!?[emoji39][emoji39]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…