Wanakagera wanavyojiona wao tofauti na mkuu wa mkoa wa Kagera anavyowaona. Nini kifanyike?

Wanakagera wanavyojiona wao tofauti na mkuu wa mkoa wa Kagera anavyowaona. Nini kifanyike?

fazili

JF-Expert Member
Joined
Jun 10, 2011
Posts
16,427
Reaction score
22,418
Nawashauri watu wa Kagera mpokee changamoto kutoka kwa mkuu wa mkoa wenu. Kwanza Chalamila hajawataja Wahaya, yeye anazungumzia watu wa Kagera. Sasa huko Kagera kuna Wanyambo, Wahaya, Wakerewe, etc. Kwanini nyie Wahaya mnafikiri kwamba watu wa Kagera ni nyie tu??

Si mnaona mnavyokosea eeh?! Sasa mtu akiwaita watu wa majungu mnachukia nini? Au mtu alisema kwamba nyie kila mtu anajifanya mwanasheria kuna wongo hapo? Chalamila anasema mnajitia wajuaji, amekosea wapi, kuna mtu asiyejua hilo?

Na zaidi ya yote mnasema Kagera ndio imetoa wasomi wengi tena maprofesa, sasa nyie mbona wakati huo huo ndio mkoa wa mwisho mwisho kiuchumi? Mnasema ardhi yenu nzuri rutuba nyingi na ziwa kubwa, mbona nyie ndio maskini wakubwa? Kuna mikoa ipo pembezoni mwa nchi haina ardhi wala wasomi lakini ipo vizuri kiuchumi, mnashindwa wapi Wanakagera? Ni uvivu, majungu au ni nini? Sasa mtu akisema Wanakagera ni majungu tu na kujifanya wajuaji anakosea wapi?

Mimi naongezea hapo kwa mkuu wenu wa mkoa; nasema acheni kiburi na majivuno kwani inachekesha kuona mtu maskini anakuwa na kibri na majivuno! Fanyeni kazi kwa bidii, acheni majungu na fitina. Pia Nendeni Kilimanjaro mkajifunze kazi na unyenyekevu!
 
Government is not your friend.
Screenshot_20230213-195503.jpg
 
Waache ujuaji kwakweli,kama ni usomi Kilimanjaro ina wasomi tangu kabla ya uhuru lakin imetulia Túlio
Kwa tafiti kule Kilimanjaro at least Kila nyumba ina MTU mwenye elimu kuanzia diploma na kuendelea Lkn Wala Haina mbambamba
Kagera MTU akiwa na PhD atatamba nchi nzima wakati Kilimanjaro PhD zipo kama utitiri wajifunze Ku relate elimu na maendleo imagine mkoa unaojiita wasomi unakuwa WA 5 kwa watoto wao kuwa na udumavu Sasa hapo Kuna elimu gani?
1676389990311.jpg
 
Back
Top Bottom