Wanakijiji Waendelea Kujenga Zahanati Mpya 16 za Vijiji Vyao: Jimbo la Musoma Vijijini

Wanakijiji Waendelea Kujenga Zahanati Mpya 16 za Vijiji Vyao: Jimbo la Musoma Vijijini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuchangia nguvukazi, fedha taslimu na vifaa vya ujenzi kwenye miradi yao ya maendeleo inayobuniwa na kuanza kutekelezwa na wao wenyewe, ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na shule mpya.

Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Kata 21 zenye Vijiji 68 na Vitongoji 374.

Huduma za Afya Jimboni mwetu:
*Zahanati 29 zinatoa Huduma za Afya (25 za Serikali na 4 za Binafsi)
*Vituo vya Afya: sita (6)
*Hospitali ya Halmashauri/Wilaya: moja (1)

Zahanati mpya 16 zinajengwa Jimboni mwetu:
Wanavijiji wako kwenye ujenzi wa zahanati mpya kumi na sita (16) kwa kutumia michango ya fedha na vifaa vya ujenzi kutoka kwa:
(i) Kaya za vijijini mwao
(ii) Mbunge wa Jimbo
(iii) Madiwani na viongozi wengine wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi
(iv) Baadhi ya wazaliwa wa vijiji na kata zenye miradi ya ujenzi
(v) baadae, Serikali Kuu hutoa michango ya kusaidia ukamilishaji wa zahanati zinazojengwa na wanavijiji.

Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura:
Kijiji cha Kaburabura ni moja ya vijiji vitatu (3) vya Kata ya Bugoji. Vijiji vyote vitatu vinatumia zahanati moja iliyoko Kijijini Bugoji.

Umbali mrefu wa kutembea kwenda kupata Huduma za Afya, ni moja ya sababu kuu iliyosababisha Kijiji cha Kaburabura kiamue kujenga zahanati yake.

Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alipiga Harambee ya kupata fedha na vifaa vya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho. Taarifa ya matokeo ya Harambee hiyo ilishatolewa, na inapatikana kwenye Tovuti ya Jimbo la Musoma Vijijini ambayo ni:
www.musomavijijini.or.tz

Michango inakaribishwa:
Wadau wa Maendeleo wanakaribishwa sana kuchangia ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kaburabura - tafadhali tuma fedha zako za mchango kwenye Akaunti ya Kijiji:

Benki: NMB
Akaunti Na: 30302300684
Jina la Akaunti: Kijiji cha Kaburabura

Picha zilizoambatanishwa hapa zinaonesha:
Wanakijiji wa Kaburabura wakichangia nguvukazi zao kwenye ufyatuaji wa matofali ya ujenzi wa zahanati ya kijiji chao.

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 23.5.2024

WhatsApp Image 2024-05-23 at 19.39.16.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-23 at 19.39.17.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-23 at 19.39.18.jpeg
WhatsApp Image 2024-05-23 at 19.39.19.jpeg
 
Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuchangia nguvukazi, fedha taslimu na vifaa vya ujenzi kwenye miradi yao ya maendeleo inayobuniwa na kuanza kutekelezwa na wao wenyewe, ikiwemo ya ujenzi wa zahanati na shule mpya.
]
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Alhamisi, 23.5.2024

View attachment 2997731View attachment 2997732View attachment 2997733View attachment 2997734
Tulifanya hivi jimboni kwangu ambapo kuna vijiji zaid ya 100 kata zaid ya 24, licha ya kwamba hatujakamilisha vyote bado, lakini tunaedelea vizur sana, kwa hatua za michango hivyo hivyo kama mlivyojipanga musoma vijijini, hamasa ya wanainchi ni kubwa mno, na kwakweli support ya govt imekua kubwa, inatia moyo na rahisi sana katika kuhitimisha miradi hiyo muhimu ya kimkakati....

Congole nyingi sana kwa mbunge Mh. Prof.Sospiter Muhongo, kwa mpango mzuri sana na kabambe, na jitihada kubwa sana za makusudi anazozifanya kwa wanaichi wa musoma vijijini kupata huduma bora za kijamii hususani za afya 🐒

God bless good people of Musoma vijijini...
 
Hongereni wananchi kwa kujua wajibu wenu kuhusu mambo yenu ya msingi. Kuna mambo majawabu yake kamwe hayawezi kupatikana Ulaya wala Marekani, kama sisi wenyewe tunaona hayatuhusu.
 
Back
Top Bottom