Wanamazingaombwe ni watu wa namna gani na kwanamna gani wanapata uwezo wa kufanya yote?

sijawah kupata jibu la hzi mada nimejaribu kufatilia sipati jibu sahih naishia kufikiria labda wanatumia majin
Hamna uchawi.ni ujanja ujanja tu.hyo elimu inafundishwa hata Google play. Kuna app zake.
 
WAENDE KWA MH rais wamshawishi AKATOE PESA ZILIZOBANWA bot ZIINGIE MTAANI WATU WAPATE UNAFUU, tuone umuhimu wao kwa taifa. (mismu huu wa krismasi)
 
naitaka na mmi mkuu hali yangu kiuchumi imekua ngumu i promise you sitaenda kwa machinga wala mamalishe ntaenda kwa wale wakubwa wakubwa
This is part of magic! White magic They call it, intended not to harm !!
 

Kwanini ziwe nguvu za giza zisiwe nguvu za Mungu?Kama tunazungumzia kutembea juu ya maji,mbona Yesu mwenyewe alitembea juu ya maji?Kuna watu wa Mungu wanafanya miujiza mpaka unashangaa kwamfano,mtu alizaliwa hatembea lakini anaguswa akiwa na miaka 50 anatembea.Kama mmoja akitambua namba yako ya account ya benki au akabashiri vichwa vya habari vitakavyoongoza katika gazeti flani neno kwa neno siku tatu kabla na mwingine akamchomoa mtu kwenye kundi akasema wewe unaumwa njoo hapa akamgusa akapona, inakuwaje mmoja akatumia nguvu za giza na mwingine za Mungu?
 
Mkuu naona nikijibu kwa kubase upande wa Mungu naona mwishowe tuyaishia kwenye mabishano ya kidini na ili tuwekane sawa hakuna budi. Ni hivi ;
Kwanza kabisa nguvu za Mungu hazifanyi kazi ili kuburudisha watu bali ni kwa utukufu wke mwenyewe. Pili ni lazima ziambatane na kumkaribisha yeye mwenyewe atende, yule aliyepale ni kama mjumbe wa udhihirisho w nguvu za Mungu kutenda kazi. Pia baada ya nguvu za Mungu kutenda kazi huambatana na shukrani na kumsifu Mungu kwa muujiza kufanyika. Kwenye Biblia Yesu aisema "na haya mtayafanya kwa jina langu" ndio maana watumishi hutanguliza kwa jina la Yesu kitu fulani kifanyike
Tukija upande wa pili wengi wanadhania ni nguvu za giza kwasababu ii jambo lifanyike hakuna haihitaji kumwalika huyo afanyaye kwa kumwita bali matayarisho yaliyofanyika tu yanatosha kuufanya uwepo wake ujae mahali apo na akatekeleza kile ukitakacho.
 
Dynamo ni bonge LA magician nimewahi kushuhudia anapaa angani kwenye moja ya vipindi VYAKE
-alipita juu ya maji pia nikajiuliza akiweka ndevu akaja bongo akapita juu ya maji si kwa wenye imani finyu kuona yesu karudi .na kuna chriss angel na yy huyu ni sheda anageuza picha kuwa real mfano alitoa grapes kwenye picha akala
 
Hakuna uchawi it's just an art of fast tricks just go Google "Breaking magicians codes biggest magic secrets revealed"
HUKU KUNAITWA KUJIFARIJI kwa lugha ya kiswahili fasaha.
 
-na kupaaa kwa dynamo vepeeeeee?
Ebu nenda YouTube tafuta video ya Breaking the magician codes, biggest magic secrets revealed wakuonyeshe wanavyopaa hakika hakuna Uchawi na kadri tukio linavyokuwa kubwa ndio maandalizi yake yanavyokuwa complicated kama la kupaa mpk helicopter au winch zinahusika!
 
Unaenda na helicopter na winch jukwaan? Sipotez MB zangu tena kwenda huko, sijawa kiaz kias hiki
 
Hakuna magic yeyote!!! Ni wepesi wa mwili, akili na uwezo wa kucontrol akili na ufikiri wa watu
Muwe mnaelezea kitafiti na si kirahisirahisi namna hiyo." kucontroo akili za watu", utacontroo vipi akili za watu kwenye hadhira bila elimu maalumu, halafu wote wakawa ni mambumbumbu kiasi cha kutokukugundua hata m1?
 
Na mimi nilikua naamini hivyo hivyo mpaka ile siku nilipoona kwenye clip jamaa kaachanishwa miguu peke yake na upande wa tumbo kwenda kichwani peke yake. Somebody aniambie ni trick gani ilitumika kama sio uchawi.
 
Uchawi,,hamna sayansi ya mtu kutoa njiwa masikioni mwake,,,,,never
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…