eliakeem
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 17,214
- 15,853
Anna Makinda alikuwa Mbunge wa Njombe na Samuel Sitta (RIP) alikuwa mbunge wa Urambo. Je wilaya ya Njombe na Urambo zikoje kimaendeleo?.
Mimi naamini maendeleo yataletwa na watu wenyewe. Serikali ina vipaumbele vyake. Dodoma kwa sasa ni makao makuu ya nchi na Serikali inajenga miundombinu ya haki ya juu, lakini Dodoma ni moja ya mikoa yenye watu maskini sana kwa nchi yetu.
Wananchi hawali barabara wala magorofa bali wanakula chakula na chakula kinatoka kwenye hela zilizoko mfukoni. Hapo ndipo Mbeya inawapiku mikoa mingi kwa kuwa hata kama haina magorofa lakini wananchi wao wana fedha.
Teh teh teh tehiii. Nenda kaskazini hasa Kilimanjaro ndo utaelewa ninachomaanisha. Kuna kipindi nilikuwa na ziara zangu kaskazini, nikajikuta niko rombo. Barabara zilizo jengwa utafikiri ya TANZAM.
Hao ulio wataja tunawashangaa. maana wamekaa miaka yote hiyo lakini hakuna walichofanikisha, kupendelea kwenu siyo dhambi.