Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 199
- 322
Siku hizi, ukitembelea mitandao ya kijamii, huenda utashuhudia video za kuvutia kama hizi: kijana wa Ulaya ya kaskazini akivaa viatu vizito vyenye picha za panda, anakunywa maji moto ili kuongeza afya; mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Marekani anafanya mazoezi ya Tai Chi kwa makini, na mama wa Kiafrika anajifunza kuimba wimbo wa pop kwa lugha ya Kichina. Hili si shindano la utamaduni wa Kichina, bali ni shughuli za “kuwa Wachina”, ambazo zinapamba moto duniani kote, na hadi sasa zimewavutia zaidi ya watazamaji milioni 100.
Shughuli hizo za “kuwa Wachina” zilianzishwa na Mmarekani mwenye asili ya Kichina. Katika video yake, alitangaza “sheria za mtindo wa maisha wa Kichina.” Sasa kuna viwango vitatu kwa watumiaji wa mtandao wa nchi mbalimbali duniani wanaoiga maisha ya kichina: Washiriki wa “kiwango cha shaba” walianza kwa kunywa maji ya moto na kuvaa viatu vizito, washiriki wa “kiwango cha fedha” wanajitahidi kuimba nyimbo za Kichina, na washiriki wa “kiwango cha dhahabu” wanaweza kufanya Baduanjin ambalo ni zoezi la kijadi la kujenga afya lenye historia ya miaka elfu kadhaa.
Kwa nini wanamtandao wa kigeni wanapenda kuiga maisha ya Wachina? Jibu ni rahisi. Hivi leo kuanzia mitindo ya mavazi hadi vifaa vya nyumbani, kutoka vifaa vya kielektroniki hadi magari ya nishati mpya, “Made in China” imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya watu duniani. Wakati watu wanaotumia vitu mbalimbali vilivyotengenezwa China, baadhi yao wana shauku ya kujua jinsi Wachina wanavyoishi maisha yao.
Kwa muda mrefu, kuhusu China, wageni wengi walijua Ukuta Mkuu, panda, na kung fu tu. Lakini sasa, utamaduni wa Kichina pia umekuwa na alama nyingi za mitindo: michezo maarufu ya Hadithi Nyeusi: Wukong, wanaserere ya mtindo LABUBU, na filamu ya Ne Zha. Vitu kama hivyo vya kitamaduni zenye ubora wa juu vimewavutia vijana wengi duniani. Kushiriki kwenye shughuli za “kuwa Wachina” kumeleta chaguo lingine la mtindo wa maisha. Mtumiaji mmoja wa mtandao kutoka Ufaransa aliyejaribu kuishi kama Wachina kwa nusu mwezi amesema, sasa ameelewa ni kwa nini marafiki zake wa China husema “polepole”, kwani kunywa maji ya moto kuliwafundisha watu kuwa na subira.
Shughuli za “kuwa Wachina” kimsingi ni hamu ya binadamu kudadisi na kujifunza kutoka kwa wengine kuhusu njia bora ya maisha. Sehemu ya kuvutia zaidi ya shughuli hizo si kuiga maisha ya Wachina, bali ni mchakato wenyewe, kwani hili ni jaribio la aina mpya la mawasiliano ya staarabu za binadamu.