Wanamuziki wa Congo wanaheshimiana sana kutoka kizazi hadi kizazi...siri ya mafanikio!

Wanamuziki wa Congo wanaheshimiana sana kutoka kizazi hadi kizazi...siri ya mafanikio!

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Nimekuwa nikiongea na wanamuziki wengi wa kutoka DRC zamani Zaire wanasema mafanikio yao yanachangiwa sana na kuheshimu mchango wa Mwalimu wako wa Music.

Mfano Mwanamuziki kama Koffie Olomide aliowafundisha music Ferre Gola na Fally Ipupa ni kwamba hawa wanamusic wawili hata siku moja hawezi kumdharau Koffie Olomide na hata siku moja hawawezi kuuza album zao bei juu zaidi ya Koffie Olomide

Kama ilivyokuwa kwa Luambo alivyomfundisha music Madilu hata siku moja Madilu haijawahi kumbeza Luambo mpaka anafariki.

Wanasema wenyewe siri hiyo ya wanamusic wa kikongo ndiyo imewafanya wengi kuwa katika viwango vizuri na hata kutokuwa na mabishano wala malumbano katika music wao wala kusikia eti wazee wamesahaulika au kulia njaa.

Hata hapa Tanzania nadhani tukiwaheshimu walimu wako wa music basi hali itakuwa nzuri tu na heshima itakuwa nzuri na music utakuwa kuliko kubezana na kuona mwalimu kwako hana maana tena baada ya mafanikio fulani uliyofikia.
 
Sina hakika sana kama ni sahihi kusema fere amefundishwa muziki na kofi, kwani amekaa quarter latin mwaka mmoja tu.
 
Kwahiyo uliongea na Koffi Olomide au Ferre Gola? Maana hao kina Luambo washakufa.
 
fere kakaa kwa koffi kidogo sana na juzi kamtukana vibaya mnooooo yeye na fally ipupa tena ferre kamuita fally shoga yaani auntie,hadi koffi olomide akshtaki polisi,koffi zamani alishakuwa na beef na papa wemba,wenge musica..king kester emeneya aligombana na papa wemba alipojitoa viva la music kuunda victoria eleison kwa kifupi hawa jamaa wana mabeef na wanalogana sana hadi kuuana ila tu zamani walikuwa na kama kautaratibu pale mmoja anapotoa style kama kwasakwasa au ndombolo ikibamba basi woooote wataiimba siku hizi wameacha hiyo kitu ,hata hapa kwetu marehemu komba alitaka kipindi flani bendi za bongo zote zitumie mtindo wa achimenengule
 
Wakongo wanamiiko kuanzia kwenye kazi zao mpaka kwenye maisha ya mtaa...,pet mokonzi,ndeng'e nini papa,sololabien,shida ni mingi kwa Duniani!
 
Back
Top Bottom