Wanamuziki wenye sifa ya unga wa ngano

1kush africa

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2016
Posts
9,552
Reaction score
13,090
2. Mr II aka Sugu; alitamba sana miaka ya 90 hadi 2000, moja ya vibao vyake matata sana ni ANA MIAKA CHINI YA 18, SUGU MOTO CHINI,

Huyu ni mmoja wa NGULI wa mziki wa bongo fleva,, Nlisoma kitabu chake kinaitwa FROM STREET TO THE PARLIAMENT,, hapo ndo nlipomjua kinagaubaga kama wanavosema watoto wa mtaa, Huyu sasa ni Mh, Joseph Mbilinyi pale mjengoni DODOMA, Huyu ameweza kubadilika kutoka mwana mziki hadi Mbunge, tayari anasifa ya unga wa ngano yaan chapati, sambusa, keki n.k

3, Profesor jay aka wa mitulinga, huyu pia ni Nguli wa bongo fleva,, tokea Hard blasterz hadi solo artist, ye ndo alibadili huu mziki ukubalike na Wazee watu wazima,

huyu alibamba sana vibao vyake CHEMSHA BONGO, BONGO DAR ER SALAAM, NDIYO MZEE, ZALI LA MENTALI n.k ila kwa sasa ni Mh, Joseph Haule pale mjengoni DODOMA, Huyu amefiti kotekote kutoka mwa mzki hadi mwana siasa pale mjengoni, huyu pia unga wa ngano ananyumbulika anapika vitu vingi,,

1, Diamond platnuzZ aka Chibu Chibude, Nasib Abdul; huyu kwa sasa ndo habari ya town, watoto wa mjini wanasema mambo ni motoooo,, kwa sasa ndo Icon ya TZ, bado anatamba na vibao vyake lukuki IYENA,MY #1,I MISS YOU,MDOGOMDOGO,FIRE,AFRICAN BEAUTY, HALLELUYAH, nk

pia ni CEO wa ;- WCB, WAFAFI TV, CHIBU PAFYUM, DIAMOND KARANGA, huyu ni unga wa ngano haswa maana mbali na mziki , amejihusisha na fursa mbalimbali za kibiashara,,

4, Ally Kiba ,, pia ana vibao lukuki vilivyotamba na vinavyotamba,, SINDERELA,NJIWA,MWANA,SEDUCE ME, Huyu nae ameanza kuwa unga wa ngano maana ana kinywaji chake cha MOFIRE,,, Ameshasoma alama za nyakati kuwa kunyumbulika ni lazima sio mziki pekeee,,
 
Anayetaka nyimbo zao aniquote, ila akubali kua atazipata kuanzia asubuhi.

Na siyo za wabana pua.
 
kama mimi sipo kwenye hiyo list "" basi utafiti wako ni batili ""...
 
Sio ustaarabu kumwita Mwanaume Mwenzio unga wa ngano



Elton John ndio ngano Kwa Kuwa anakandwa Na anakandika
 
Sio ustaarabu kumwita Mwanaume Mwenzio unga wa ngano



Elton John ndio ngano Kwa Kuwa anakandwa Na anakandika
kiswahili lugha yetu, sijamaanisha ivo,,

kiswahili ulipata ngap
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…