Wananchi 121 wa Uganda watoweka

Wananchi 121 wa Uganda watoweka

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kampala, Uganda. Jeshi la Polisi nchini Uganda limesema kuwa limepokea taarifa 48 za watu kutoweka na kuingizwa katika biashara haramu ya binadamu nchini kwa kipindi cha miezi sita iliyopita.

Hata hivyo, inaaminiwa kuwa watu 121 wamehusishwa katika biashara hiyo. Inaripotiwa kuwa watu 78 walisafirishwa nje ya nchi huku wengine 43 wakitoweka katika mazingira ya kutatanisha nchini humo.

Polisi wanasema wamefanikiwa kuwaokoa watu hao waliotoweka. Moses Binoga kutoka kitengo cha kushughulikia matukio ya watu kupotea, amesema idadi kubwa ya watu waliotoweka na kupatikana ni wasichana.

Wasichana wengi waliohojiwa wamekuwa wakilalamikia kuwa wamekuwa wakinyanyaswa kingono wanapopelekwa katika mataifa ya Mashariki ya Kati.



Chanzo: mwananchi
 
Back
Top Bottom