Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wakati kwao wewe linaweza kuwa jambo la kawaida kuona Shule zikiwa karibu yako, kwa wakazi wa kata ya Nyamagoma shule ya Sekondari ilikuwa inapatikana umbali wa zaidi ya Kilomita 40 ambazo watoto walilazimika kuzitembea kila siku kuitafuta ndoto yao ya maisha ya baadaye.
Katika eneo lenye Milima, Mabonde na ukosefu wa Usafiri, elimu ya SEKONDARI ilikuwa ni Mateso makubwa kwao na wengi hawakuweza kuhitimu kidato cha nne.
Ilipofika mwaka 2020, Mhe. Ndaisaba George Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara na Diwani wa Kata hiyo Mhe. Laurent Msongalele walitoa ahadi ya kuwajengea Shule ya Sekondari iwapo wangechaguliwa kuongoza katika nafasi walizoziomba.
Kwa Uwezo wa Mungu, Mbunge Ndaisaba Ruhoro na Diwani walishinda na kumkimbilia Mama wa Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alikubali na kutoa TZS 584,000,000 kufanikisha ujenzi wa Shule hiyo.
Ujenzi ulipokamirika, wananchi walimuomba Mbunge Ndaisaba George Ruhoro kuwasaidia kufanya Sherehe ya Kuwapongeza viongozi wao akiwemo Rais Samia ambaye ametoa fedha za kufanikisha ujenzi wa shule hiyo. Mbunge Alikubali na kutoa TZS 5,600,000 na Mchele kilo 100. Wananchi wamechangia kilo za mchele 650kg.
Aidha, Ng’ombe 4 wamechinjwa na wananchi zaidi ya 2,300 walihudhuria na kupata chakula cha kutosha sana sambamba na kumpongeza Rais, Mbunge na DIWANI kwa kuwafanyia kazi Nzuri sana.
Wananchi hao wameadhimia kuhakikisha wanawachagua viongozi wao hawa hawa ambao wameweza kutatua kero zao.
Attachments
-
WhatsApp Image 2024-12-08 at 00.57.38.jpeg156.6 KB · Views: 4 -
WhatsApp Image 2024-12-08 at 00.57.34.jpeg226.3 KB · Views: 3 -
WhatsApp Image 2024-12-08 at 00.57.31 (1).jpeg162.2 KB · Views: 2 -
WhatsApp Image 2024-12-08 at 00.57.23 (1).jpeg106.2 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-12-08 at 00.57.12 (1).jpeg170.7 KB · Views: 4