Baadhi ya wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam wamesema, baada ya kukamilika kwa mchakato wa kujiandikisha kwenye Daftari la Mkazi la Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni wakati wa wananchi kujiandaa kwenda kupiga kura ili kuwachagua Viongozi watakaowaletea maendeleo katika maeneo yao.