Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Katika hali inayoonyesha kuwa pigo kwa utawala wa Rais Felix Tshisekedi wa DRC, Wananchi wa Congo 🇨🇩 wamemshangilia Rais Kabila wakati Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Jean Pierre Bemba akihutubia leo Kinshasa
Soma Pia: Aliyekuwa Rais wa DRC, Kabila, Kuongoza Muungano Mpya Utakaochukua Nafasi ya AFC/M23
Siku ya Jumatatu Joseph Kabila, alitangaza kuchukua uongozi wa jukwaa jipya la kisiasa na kijeshi linalojulikana kama Front for the Refoundation of the Nation (FRN).
Muungano huo unajumuisha viongozi wakuu kutoka kundi la waasi la AFC/M23 na unajipanga kupinga serikali ya Kinshasa chini ya Rais Tshisekedi.

Dhamira ya Front for the Refoundation of the Nation ni kuunganisha na kuratibu majeshi yote ya upinzani ili kukomesha utawala wa kibabe—kwa kutumia njia yoyote inayowezekana, ikiwa ni pamoja na nguvu—na kuchora mwelekeo mpya pamoja na kuunda fursa mpya kwa nchi