Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 21,741
- 26,735
Wananchi hawa tunaishi nao ila tumewabagua kwa kuwaita "viziwi, bubu"! Kwenye maisha yetu ya kila siku huwa hatuwashirikishi kwenye maongezi, tunawabagua japo tumezaliwa nao tumbo moja!
Umefika wakati sasa tuwaite mezani tuongee nao kwa kutumia lugha moja bila kuwepo mtu wa kati, ili kufanikisha hili serikali ianzishe somo la lugha ya alama shuleni ambapo nalo litapewa uzito kama kiswahili na kiingereza. Wananchi wote tukijua lugha ya alama tutakuwa tumewapa furaha ambayo wameikosa tangu wazaliwe kwa kuwa tunawabagua bila kosa.