PreGE2025 Wananchi Jimbo la Vunjo wamtaka Mbunge wao Charles Kimei, kuendelea kutetea kiti cha Ubunge

PreGE2025 Wananchi Jimbo la Vunjo wamtaka Mbunge wao Charles Kimei, kuendelea kutetea kiti cha Ubunge

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jimbo la Vunjo limeendelea kuwa miongoni mwa majimbo yenye msisimko mkubwa kila uchaguzi mkuu unapokaribia, lakini awamu hii hali inaonekana kuchukua sura tofauti, baada ya mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Dkt Charles Stephen Kimei, kuonekana kupigiwa upatu na wananchi walio wengi kutetea tena nafasi hiyo

Kwa mujibu wa maoni yaliyokusanywa na waandishi wetu katika kata mbalimbali za jimbo hilo, wananchi wengi wameeleza kuwa Dkt Kimei ameleta mwelekeo mpya wa uongozi wa uwazi, uwajibikaji na utendaji wa kazi unaoonekana

Wengi wamemwelezea kama mbunge anayewasikiliza na kuwa karibu na jamii, huku akitajwa kuwa "Mbunge wa vitendo, si maneno."

Katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wake, Dkt Kimei amesimamia miradi kadhaa mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, uboreshaji wa shule za msingi na sekondari, ujenzi wa barabara za vijijini, pamoja na usambazaji wa umeme kupitia mradi wa REA

Pia ameendelea kushiriki mijadala ya Bunge kwa nguvu, ambapo ameuliza zaidi ya maswali 100 na kuchangia hoja muhimu zinazogusa maisha ya wananchi wa Vunjo

Isitoshe, mbunge huyo ameweka rekodi kwa kuwa miongoni mwa viongozi wachache wanaorejea jimboni mara kwa mara kwa ajili ya kusikiliza wananchi, kufuatilia utekelezaji wa miradi, na kushiriki mikutano ya hadhara ya uwajibikaji hali ambayo imewafanya wananchi wengi kuona ni haki kumpa nafasi ya kuendeleza alipoishia

Hata hivyo, hali ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) si ya kubeza, kwani tayari kuna idadi kubwa ya makada wa chama hicho wanaotajwa kuonesha nia ya kugombea nafasi hiyo kupitia vikao vya ndani vya chama

Wananchi kutoka maeneo ya Kirua, Kahe, Njiapanda, Mamba, Makuyuni, Mwika na Marangu wameeleza kuwa japokuwa ushindani ndani ya chama ni ishara ya demokrasia, hawana mashaka na uwezo wa Dkt Kimei kuendelea kuwakilisha vyema Jimbo la Vunjo endapo atapewa tena nafasi hiyo

Ikiwa ni takribani siku tano kabla ya mchakato rasmi wa kuchukua na kurejesha fomu za ubunge kuanza ndani ya CCM, macho na masikio sasa yameelekezwa Vunjo jimbo ambalo linabeba historia, ushindani, na matarajio

20250627_144443.jpg
 
goooooooooooooooooooooodiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii kimya kimya
 
Wameshatembezewa ankara, uzuri wa uchaguzi wa Tz. Unaenda tu kipindi cha uchaguzi, inawapa pesa, wanasahau shida zote za miaka 5.
 
Back
Top Bottom