Wananchi Kagera walia na uchafu mtaani

Wananchi Kagera walia na uchafu mtaani

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Baadhi ya wakazi wa Kata za Bilele na Bakoba katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, wameiomba serikali kuwachukulia hatua kali wananchi ambao wanazalisha taka na kuzitupa katika Mto Kanoni, maana kufanya hivyo wanahatarisha afya na usalama wao.

Wakazi hao wamesema kuwa tatizo hilo linasababisha taka kuzagaa hovyo na kwamba asilimia kubwa ya wanaofanya vitendo hivyo wanafanya makusudi, maana ni maeneo machache ambayo hayana sehemu za kukusanyia taka.

Wakizungumzia tatizo hilo wenyeviti wa mitaa ya Buyekera Asili na Mtoni wamewataka wananchi kuacha tabia hiyo mara moja na badala yake watumie maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutupa taka.

Diwani wa Kata Bakoba, Shaban Rashid amedai wakaobainika kuendelea na vitendo hivyo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria za halmashauri.

Chanzo: EATV
 
Back
Top Bottom