MTANZANIA620
Senior Member
- Jun 20, 2023
- 105
- 116
Wananchi wa Kata ya Kahe Mashariki, wakiongozwa na wazee wa kata hiyo, wamempongeza Mbunge wa Jimbo la Vunjo, Mhe. Dkt. Charles Stephen Kimei kwa kazi nzuri aliyoifanya katika kipindi cha mwaka 2020 - 2025, kwa kumzawadia ndafu (mbuzi dume) kama ishara ya heshima na shukrani.
Wakizungumza wakati wa hafla hiyo, wazee wa kata hiyo wakiongozwa na Ndg Silas Msumanje, Ndg Solomon Kimati na Ndg Rasuli Kitia walieleza mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Dkt. Kimei kupitia serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan. Miongoni mwa mafanikio hayo ni:-
Ujenzi wa zahanati katika vijiji vya Kochakindo na Ghona
Ujenzi wa jengo la afya ya uzazi, mama na mtoto katika zahanati ya Kyomu
Ushawishi uliofanikisha upatikanaji wa shilingi bilioni 7 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Chekereni - Kahe - Mabogini
Ushawishi wa serikali kulijenga bwawa la Urenga kwa ajili ya huduma ya maji na kilimo
Wazee hao walimpongeza Dkt. Kimei kwa uongozi wake wa karibu na wananchi na kumtaka kuchukua tena fomu ya kugombea ubunge kwa kipindi kingine, huku wakiahidi kumuunga mkono kwa dhati.
Kwa upande wake, Dkt. Kimei aliwashukuru wananchi na jamii ya Kahe Mashariki kwa kuwa mstari wa mbele katika maendeleo, na kuahidi kuendelea kuwa mwakilishi mwaminifu, mchapakazi na mwenye kusikiliza wananchi wake.
"Nawashukuru kwa moyo huu wa upendo na mshikamano. Tumefanya mengi kwa pamoja, na bado safari ya maendeleo inaendelea. Nipo pamoja nanyi," alisema Dkt. Kimei.
Pia soma Pre GE2025 - Hawa wabunge wanaochangiwa fedha za kuchukulia fomu za ubunge ni kwamba wamefanya makubwa huko jimboni au ni uchawa na kujipendekeza?