A
Anonymous
Guest
Wananchi wa Vijiji vya Simambwe, Shibolya, Usoha Njiapanda, Ilembo Usafwa na Galijembe vilivyopo Kata ya Tembela, Wilaya ya Mbeya, walilazimika kuchangishwa michango kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Afya Simambwe kutokana na changamoto ya upatikanaji wa huduma za matibabu ambapo vijiji vyote hutegemea Zahanati ya Simambwe ambayo haikidhi idadi ya watu wanaohitaji huduma za afya.
Upatikanaji wa huduma katika zahanati hiyo umekuwa si wa uhakika kwani mara tu muda wa kazi unapoisha pamoja na siku za weekend hakuna huduma zozote za afya zinazotolewa licha ya uwepo wa nyumba za madaktari ambao pia hawaishi katika nyumba hizo, hivyo kusababisha changamoto kwa wanawake wajawazito na wanaougua nyakati za usiku kukosa huduma za haraka na kusababisha kupoteza maisha ya watu wengi.
Kutokana na Changamoto hiyo wananchi waliaminishwa kuwa wachangie ujenzi wa kituo cha afya mpaka jengo litakapofikia mtambaa wa panya na baadaye serikali itamalizia ujenzi wa kituo hicho, lakini ni zaidi ya mwaka sasa hali ni tofauti jengo lililochangiwa na wananchi ni kama limetelekezwa na hakuna dalili yoyote ya serikali kusaidia ujenzi huo huku wananchi wakiendelea kuhangaika kupata huduma za afya.
Hata hivyo kabla ya ujenzi kuanza wananchi walichangishwa fedha kwa ajili ya kununua matofali ya kujengea kituo hicho, ambayo yalitelekezwa na kuacha yakiharibika kwa kigezo kuwa hayakukidhi ubora wa kujengea kituo hicho.
Tuna changamoto nyingi lakini hatujawahi kumsikia mbunge wetu wa Mbeya Vijijini akitusemea wananchi wake bungeni ili changamoto zetu zitatuliwe, tunaiomba serikali itusaidie kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Simambwe ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya katika kata ya Tembela ambayo ina watu zaidi ya 10,000 ambao wanahangaika kupata huduma za afya kutokana na zahanati kushindwa kumudu idadi hiyo.