GE2025 Wananchi Kati Unguja Walalamikia Serikali kwa Kunyang’anywa Ardhi Zao kwa Ajili ya Wawekezaji

GE2025 Wananchi Kati Unguja Walalamikia Serikali kwa Kunyang’anywa Ardhi Zao kwa Ajili ya Wawekezaji

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Wananchi wa wilaya ya kati Unguja wamelalamikia Serikali wakidai ya kunyanganywa ardhi zao na kupewa wawekezaji.

Akizungumza katika mkutano maalumu wa kusikiliza shida za wananchi, Mkaazi wa eneo hilo, Ali Suleiman Abdallah amesema wao wanasumbuliwa na uwekezaji ambapo baadhi ya maeneo yao yamechukuliwa sehemu kubwa.

Amesema licha ya kuwa wamechukuliwa sehemu ya shamba lao lakini baada ya muda kikachukuliwa eneo lao jengine kubwa zaidi.

"Tunasikia kuwa baada ya uchaguzi litakuja kuchukuliwa eneo lile kwa hivyo tunakuombeni mkae kuzungumza na wahusika" amesema Ali Suleiman.

Katika kuonesha kutoridhishwa na hatua hiyo amesema hata kama watalipwa basi yeye uamuzi wake ni kutokukubali kulipwa kwani shida yao wanataka maeneo yao yabaki mikononi mwao na sio kunyanganywa.

 
Katika kuonesha kutoridhishwa na hatua hiyo amesema hata kama watalipwa basi yeye uamuzi wake ni kutokukubali kulipwa kwani shida yao wanataka maeneo yao yabaki mikononi mwao na sio kunyanganywa.
Wamasai walisema hivyo wakapewa kipigo cha hatari. Ngoja tuone
 
Back
Top Bottom