Baadhi ya wananchi wa Mbeya Mjini wamesema hawajamtuma bungeni Mbunge wao Dk. Tulia Ackon kutetea wezi na walanguzi wa kuwakamua wananchi kupitia biashara ya mafuta.
Hii ni baada ya wachangia kuwashambulia wananchi wa Mbeya kwamba ndiyo wamesababisha tatizo hili kwa kuwa maamuzi ya Spika Tulia ni uwakilishi wa sauti yao wananchi wa Mbeya waliompa dhamana bungeni.
Wakichangia mjadala kwenye makundi mbalimbali ya WhatApp baada ya taarifa ya kupanda kwa bei ya mafuta na kukumbishia namna Spika alivyokuwa ameshauriwa na wabunge kuunda tume kuchunguza upigaji unaofanywa kwenye biashara ya mafuta.
Wananchi wamesema " Tulia ni Mbunge wetu lakini hilo hatukumtuma Kosa ni lake siyo la wananchi kwani aliwauliza wananchi? alisema mmoja wa mkazi wa Mbeya Mwakasasa.
Mwingine akichangia mjadala huo amesema 'Mbunge ndiye alikataa aisee sio wananchi (hakufikiria dhamana ya umma alifikiria dhamana ya kisiasa hapa aliamini kuwa akiruhusu tume iundwe moja kwa moja chama kitamtafsiri kuwa ana mhujumu Mwenyekiti wa CCM Samiah Suluhu Hassan kuwa Serikali yake imeshindwa kudhibiti mfumko wa bei" amesema Ndugu Mwaipaja.