Wananchi Mikoa ya Kusini wapo hoi bin taaban kiuchumi. Ni baada ya uporaji wa KOROSHO zao 2017

Wananchi Mikoa ya Kusini wapo hoi bin taaban kiuchumi. Ni baada ya uporaji wa KOROSHO zao 2017

Kinoamiguu

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2018
Posts
11,936
Reaction score
15,196
Wandugu,

Hali ni mbaya Mikoa ya kusini, Pwani, Lindi na Mtwara. Zao la KOROSHO siyo mkombozi wao tena. Ikumbukwe hapo mwishoni mwa mwaka 2017 serikali ilitangaza ununuzi wa zao la KOROSHO kwa kisingizio cha kukomesha unyonyaji kwa WAKULIMA wa zao hilo.
Kwa mujibu wa wakazi wa huko tangu wakati huo hali haijatengemaa mpaka sasa ni vilio.

Huu ni wakati wa kuandaa mashamba. Kabla ya uporaji ule wananchi walikuwa wana namna zao za kukopeshana. Mfano unapewa salpher utakuja kurudisha KOROSHO ilikuwa kawaida. Mabenk nayo hayakuwa nyuma, unakopeshwa ukija kulipwa pesa unapita bank wanakata cha kwao maisha yanaenda. Baada ya serikali ya bwana mkubwa kuingilia sasa kila kitu kimekwama. Wakopeshaji hawatoi mikopo tena kwani wanaogopa kuambiwa waoneshe mashamba tena na wanaishi wenye magwanda.

Zao la KOROSHO ambalo lilikuwa mkombozi Mikoa ya kusini sasa limegeuka shubir halina soko tena. Wapo waliouza kg 50 lakini analipwa kilo mbili mbili. Wakamdai nani? Siyo vyama vya ushirikiano AMCOS wala nini vyenye lakusema juu ya malipo yao! Wasemeje nae mchumi mkuu wa taifa ameshaamua.

Siyo KOROSHO tu. Kabla ya 2015 kusini kulikuwa na mazao matatu. Mbaazi kwisha kazi, kazi, korosho na ufuta yote kwisha kazi.
KUONESHA KWAMBA AMEHARIBU NA KUKERA WATU 2021 HAJAENDA KUPIGA KAMPENI HUKO KUSINI.

Je. Wakusini waendelee kuimba hapa kazi tu? Wamevuna walichopanda? Ni kivuli na majivuno ya mtawala?
 
Afu Jiwe kajikausha kama hakijatokea kitu
 
Sio Mitano tena ni milele kabisa tafadhali....
Hapa kazi tu....
Uchumi wa kati.....
Nchi hii ni tajiri sana....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu....

Unaijua vieite wewe...
Sisi tunatembelea mavieitee
 
Kuna kakikundi ka wapuuzi wajinga, wapumbavu, wenye chuki, inferiority complex, roho mbaya, kanajiita inner circle ndo kanaitaabisha nchi.
 
Kiukweli mikoa ya Lindi na Mtwara hapafai kabisa toka zao la korosho lilipozingua
 
Tunataka Tanzania iwe kama urayaaaa, rindi iwe kama carufonia, dodoma iwe kama dubai ..au nasema uwongo ndugu zangu?
 
Zaman si mlikuwa mna wanywesha soda ya fanta mbuzi sasa safari wote yaaan mwenye mbuzi na mbuzi wake watakunywa maji ya kisima 😂😂😂😂 alululululululuuuuuuuu

Hapa ndipo nakumbuka zile modal za sustainable livelihood za DFID
 
Back
Top Bottom