KERO Wananchi Mkundi Morogoro hatujaunganishiwa maji kwenye nyumba wakati miundombinu iko tayari

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Swali kwa Mh Waziri wa maji,

Kuna shida gani mpaka leo maji hayajaunganishwa majumbani wakati tenki lipo tayari, mashine ipo tayari, mabomba makubwa yameshasambazwa mitaani, Wananchi tunalazimika kwenda kufata maji mbali kwa watu wanaouza.

Pia Rais Samia alishawahi kupita na kutuambia Wananchi wa Mkundi hatumdai, lakini zimepita siku nyingi huduma ya maji haijaanza kupatikana ili tuunganishiwe maji majumbani kwetu

Je, kuna shida gani inayosababisha wananchi wa Mkundi Morogoro tuendelee kuteseka kwa adha ya maji ilihali miundo mbinu ipo tayari?

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo imesababisha ugumu kwa Wananchi wa Kata ya Mkundi kuuziwa maji kwa shilingi 500 mpaka 700 kwa dumu na tunayapata kwa kuchelewa na usiku sana.

=========================
Screenshot 2025-03-24 092607.jpg
 
Kijiji kinaitwa Mkundi, watu wa kanda ya kati tukipita hapo tunaposoma kile kibao chao barabarani huwa tunacheka sana na kushangaa jina hilo
 
Swala la maji nchin n tatizo kubwa sna hv idara ya maji kuna wataalam kwl au ndo vishoka.skuhz kuunganishwa maji na upate meter lazm utoe cha juu lasivyo utaambiwa meter zmeisha.wizara ya maji lazm ijitathmin kuna madudu meng sna yanaendelea
 
Swali kwa Mh Waziri wa maji,

Kuna shida gani mpaka leo maji hayajaunganishwa majumbani wakati tenki lipo tayari, mashine ipo tayari, mabomba makubwa yameshasambazwa mitaani, Wananchi tunalazimika kwenda kufata maji mbali kwa watu wanaouza.

Pia Rais Samia alishawahi kupita na kutuambia Wananchi wa Mkundi hatumdai, lakini zimepita siku nyingi huduma ya maji haijaanza kupatikana ili tuunganishiwe maji majumbani kwetu

Je, kuna shida gani inayosababisha wananchi wa Mkundi Morogoro tuendelee kuteseka kwa adha ya maji ilihali miundo mbinu ipo tayari?

Kutokana na kuwepo kwa changamoto hizo imesababisha ugumu kwa Wananchi wa Kata ya Mkundi kuuziwa maji kwa shilingi 500 mpaka 700 kwa dumu na tunayapata kwa kuchelewa na usiku sana.

=========================
View attachment 3281534​
Kama Vipi Hamieni Burundi
 
Back
Top Bottom