Pre GE2025 Wananchi na viongozi wa dini wataka lililokuwa Jimbo la zamani la Zitto Kabwe, Kigoma Mjini ligawanywe mara mbili

Pre GE2025 Wananchi na viongozi wa dini wataka lililokuwa Jimbo la zamani la Zitto Kabwe, Kigoma Mjini ligawanywe mara mbili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Mnamo Februari 26, Mwaka huu Tume Huru ya Uchaguzi (INEC) kupitia Mwenyekiti wake Jaji wa Rufani, Jacobs Mwambegele ilitangaza kuanza kwa mchakato wa kuchunguza, kugawa au kubadili majina ya majimbo ya uchaguzi ambapo Tume hiyo imeanza kupokea mapendekezo hayo kuanzia Februari 27, 2025 hadi Machi 26, 2025 kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 74(6)(c) na ibara ya 75(4), sheria Na. 2 ya Tume Huru ya Uchaguzi kifungu cha 10(1)(d) ya 2024. Masharti ya kanuni ya 18(1) ya kanuni ya TumenHuru ya Uchaguzi ya 2024.

Mkoa wa Kigoma una majimbo 8 , Kigoma Mjini , Kigoma Kusini ,Muhambwe ,Buhigwe,Buyungu ,Kigoma Kaskazini, Kasulu Mjini na Kasulu Vijijini.

Wananchi na viongozi wa Dini wa Mkoa wa Kigoma wamekuwa na maoni tofauti majimbo kadhaa yagawiwe ikiwemo Jimbo la Kigoma Mjini wakitaka yawe mawili Jimbo la Ujiji na Jimbo la Kigoma Mjini, Jimbo lingine ni Kasulu Vijijini (Jimbo la Kijijini) lenye idadi ya watu 537,767 na Kata 21 wakitaka yawe majimbo mawili sababu ya ukubwa na idadi ya watu , Jimbo lingine ni Kigoma Kusini (Jimbo la Kijijini) lenye idadi ya watu 458,353 na Kata 16 wakitaka yagawiwe mawili sababu ya idadi ya watu wengi na ukubwa wa Jimbo hilo.

Kulingana na vigezo vya Tume huru ya uchaguzi ili kugawa jimbo ni Jimbo la kijijini kuwa na idadi ya watu zaidi ya 400,000 na Jimbo la mjini kuwa na zaidi ya watu 500,000 na vigezo vingine vya kiuchumi na kijeografia.


 
Back
Top Bottom