Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Hawa watekaji walianza kuwateka wanaharakati. Kwa kawaida wanaharakati huwa hawana wafuasi rasmi. Watekaji walifanya hivyo kupima mwamko na nguvu ya wananchi pale inapotokea mmoja wao anafanyiwa uharamia. Wakataka kuona, Watamzania watafanya nini dhidi yao.
Matokeo: Watanzania, kama nyumbu wanapomwona mwenzao amekamatwa na simba, wao hupumua wakiamini kuwa sasa wapo salama, bila kujua kuwa njaa ya simba haitamalizwa na kumla yule nyumbu mmoja, kesho itabidi akamatwe mwingine, na kadiri wanavyozidi kukamatwa wenzako, zamu yako inazidi kukaribia.
2) Watekaji walipojiridhisha kuwa kumbe Watanzania, kama walivyo nyumbu, hawaumizwi na madhira ya mwananchi mwenzao mmoja, wakaamua waende kwa waliokusudia, huku wakijua kuwa wananchi hawatafanya lolote.
3) Wakawateka viongozi wa ngazi za chini wa CHADEMA. Watekaji wanajua kuwa CHADEMA ina wanachama, wafuasi na wapenzi. Walifanya hivyo ili kuona, je hao wanachama, wapenzi na wafuasi wa chama watafanya nini?
Matokeo: Nao wakakaa kimya, wakafanya kama nyumbu wafanyavyo. Hapo watekaji wakajipa uhakika kuwa wanaweza kuendelea kuteka na kuwaua viongozi wa ngazi za chini wa CHADEMA, bila bugdha yoyote. Lakini wakawa hawana uhakika wakiwagusa viongozi wa kitaifa.
3) Jaribio lao la kwanza wamemteka na kisha kumwua msaidizi wa katibu mkuu wa CHADEMA Taifa. Wanasubiria kuona kama kutakuwa na reaction kutoka kwa wanachama, wapenzi na wafuasi wa CHADEMA, halikadhalika kutoka kwa wananchi. Hili likipita kimya, watakuwa na uhakika wa kumteka au hata kumwua Mbowe, Lisu, Mnyika au kiongozi mwingine yeyote bila ya kuwa na hofu yoyote.
NB: Lakini wanachama wa vyama vingine, viongozi wa vyama vingine vya upinzani, na hata ndani ya CCM, kwa ujinga nao wanafanya kama nyumbu. Wakiamini kuwa wanaotafutwa ni CHADEMA pekee, wakati kiuhalisia tukilikubali hili, huu ndio utageuka na kuwa utamaduni mpya wa utawala nchini Tanzania. Hata ukiwa ndani ya CCM, ukakosoa kama alivyofanya Mpina, ujue utekaji na kisha mauaji vinakuhusu. Hata ukiwa kwenye Serikali ya umoja Zanzibar, ukakosoa chochote, ujue utekaji na mauaji vinakuhusu. Hata ukiwa ndani ya Serikali, ukaonekana ni tishio kwa watu fulani, ujue utekaji na mauaji vinakuhus.
Pia soma: Ally Mohamed Kibao auawa na mwili kutelekezwa Ununio ukiwa umeharibika sana
WITO:
Kama wewe mwenyewe hutaki kutekwa, hutaki ndugu na mwanafamilia wako kutekwa na kuuawa, wakati wa kuzuia ni huu wa sasa ambao bado unapumua. Ukishatekwa, umeuawa, huna nafasi ya kuuzuia utekaji na mauaji holela yanayoendelea nchini mwetu sasa, na yanayozidi kuota mizizi.
Viongozi wa dini, walio wengi wapo kimya dhidi ya uovu huo, yawezekana na wao wamekuwa kama nyumbu, wakiamini huo uharamia utaishia kwa CHADEMA. Lakini wajue kuwa utaratibu huu unaoendelea kuota mizizi, watekaji hawataona shida kumteka na hata kumwua kiongozi yeyote wa dini atakayejaribu kukosoa chochote.
Wananchi tujue kuwa kila kitu huanza kwa udhaifu, kisipobugudhiwa au kukataliwa, kadiri siku zinavyoenda, kitazidi kukua na kujiimarisha. Utaratibu huu mpya wa kuwateka na wakati mwingine kuwaua wakosoaji, ulianza kidogo kidogo, pengine utasikia tukio 1 kwa mwaka, lakini siku ziendavyo, matukio yanazidi kuongezeka, hii ni kudhihirisha kuwa watekaji na mfumo wa utekaji na mauaji, vinazidi kujijenga na kujiimarisha. Siku za huko nyuma, wakosoaji walikuwa wanakamatwa na kufunguliwa kesi za kubambikizwa. Sasa wakosoaji wanatekwa, kisha kuuawa mafichoni. Itakuja wakati, wakosoaji watakuwa wanauawa mbele ya macho ya wananchi wote, na sisi, kama nyumbu, tutabakia tunatizama kusubiria siku ya kwetu.
Tunamwomba Mungu utusaidie Watanzania, tuache unafiki, tuuheshimu na kuulinda uhai wetu na wa wenzetu kwa gharama yoyote ipasayo huku Mkono wako wenye nguvu ukitupatia ujasiri na ushidi dhidi ya uovu na waovu.