Wananchi onyesheni ushirikiano kwa Serikali kukabiliana na COVID 19

Kanamusi

Member
Joined
Apr 9, 2020
Posts
22
Reaction score
65
Kutokana na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali kupitia wizara ya afya na vyombo vya usalama kudhibiti maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID 19), Kumekuwepo na tabia ya raia wa kigeni kuingia nchini kinyemela kwa njia za panya. Raia hao wanatumia njia za panya kukwepa utaratibu uliowekwa na serikali wa kufikia kwenye Quarantine kwa muda wa siku 14 kwaajili ya uangalizi.

Katika mazingira kama hayo, imekuwa ni ngumu kuwafanyia vipimo na hivyo kujichanganya na raia wa kawaida nchini bila kugundulika kama wana maabukizi au la!.

Hivyo basi nitoe wito kwa wananchi wote mnaokaa maeneo jirani na mipaka ya nchi yetu kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya raia yeyote kutoka nchi jirani aliyeingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu wa kawaida wa kukaa karantini kwa siku 14.

Lengo ni kuhakikisha tunakomesha maambukizi kutoka nje ili tubaki na kazi moja tu ya kushughulikia maambukizi ya ndani.

Wananchi wa mikoa ya mara hususani sirari , wananchi wa kigoma, kagera, wananchi wa visiwa vya ukerewe vinavyopakana na uganda na maeneo yote kwa ujumla tunaomba ushirikiano wenu.

Vile vile, nitoe rai au ushauri kwa wazazi wote siku ya kesho na keshokutwa (jumapili na jumatatu) ya pasaka msiruhusu watoto kwenda mitaani kuchangamana na watoto wengine, aidha washerehekee sikukuu ya pasaka wakiwa majumbani mwao ili kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Kwa pamoja tukiamua tunaweza, muda wa kuchukua tahadhari ni sasa. Corona inaepukika.

Nawatakia siku njema na maandalizi mema ya pasaka.
 
IMG_20200411_044022.jpg
 
Sisi tusio mipakan ndo hivyo tunaonesha ushirikiano, tunanaw mikono hadi inakua meupe au ushirikiano UPI mwingine

Sent using Jamii Forums mobile app
nakupongeza kwa kutekeleza maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya ya kunawa mikono kwa sabuni na maji ya kutiririka. Mambo mengine ya kuzingatia ni kuepuka mikusanyiko isiyo na umuhimu na kusalimiana kwa kushikana mikono. Sambamba na hayo yote hakikisha unatoa elimu pia kwa familia yako na jamii inayokuzunguka juu ya namna ya kujikinga na maambukizi haya ya virusi vya corona.
 
Kutokana na jitihada mbali mbali zinazofanywa na serikali kupitia wizara ya afya na vyombo vya usalama kudhibiti maambukizi ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona (COVID 19), Kumekuwepo na tabia ya raia wa kigeni kuingia nchini kinyemela kwa njia za panya. Raia hao wanatumia njia za panya kukwepa utaratibu uliowekwa na serikali wa kufikia kwenye Quarantine kwa muda wa siku 14 kwaajili ya uangalizi.

Katika mazingira kama hayo, imekuwa ni ngumu kuwafanyia vipimo na hivyo kujichanganya na raia wa kawaida nchini bila kugundulika kama wana maabukizi au la!.

Hivyo basi nitoe wito kwa wananchi wote mnaokaa maeneo jirani na mipaka ya nchi yetu kutoa taarifa kwa vyombo vya ulinzi na usalama dhidi ya raia yeyote kutoka nchi jirani aliyeingia nchini kinyemela bila kufuata utaratibu wa kawaida wa kukaa karantini kwa siku 14.

Lengo ni kuhakikisha tunakomesha maambukizi kutoka nje ili tubaki na kazi moja tu ya kushughulikia maambukizi ya ndani.

Wananchi wa mikoa ya mara hususani sirari , wananchi wa kigoma, kagera, wananchi wa visiwa vya ukerewe vinavyopakana na uganda na maeneo yote kwa ujumla tunaomba ushirikiano wenu.

Vile vile, nitoe rai au ushauri kwa wazazi wote siku ya kesho na keshokutwa (jumapili na jumatatu) ya pasaka msiruhusu watoto kwenda mitaani kuchangamana na watoto wengine, aidha washerehekee sikukuu ya pasaka wakiwa majumbani mwao ili kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima.

Kwa pamoja tukiamua tunaweza, muda wa kuchukua tahadhari ni sasa. Corona inaepukika.

Nawatakia siku njema na maandalizi mema ya pasaka.

Mkuu sasa hivi maambukizi ya ndani nayo yashashika kasi tena.

Kwa wageni sasa tunakumbuka shuka kumeshakucha.
 
Mkuu sasa hivi maambukizi ya ndani nayo yashashika kasi tena.

Kwa wageni sasa tunakumbuka shuka kimeficha.
Ni kweli, ndio maana nikasema wananchi waonyeshe ushirikiano kwa kufichua taarifa za raia wa kigeni wanaoingia nchini kinyemela ili tubaki na kazi moja tu ya kushughulika na maambukizi ya ndani
 
Nawakumbusha wazazi wote kutowaruhusu watoto kutoka kwenda kuchangamana na watoto wengine mitaani badala yake wakae na kusherehekea sikukuu ya pasaka wakiwa nyumbani na endapo kutakuwa na ulazima wa kutoka hakikisheni wanakuwa chini ya uangalizi wenu. Nawatakia utekelezaji mwema
 
Back
Top Bottom