Wananchi tunataka Katiba Mpya ndio maana tulishiriki kutoa mapendekezo Tume ya Warioba

Wananchi tunataka Katiba Mpya ndio maana tulishiriki kutoa mapendekezo Tume ya Warioba

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2021
Posts
3,085
Reaction score
4,890
Hakika haiingii akili kumsikia katibu mkuu wa CCM eti anasema wananchi hawataki katiba mpya. Bw. Chongolo napenda nikukumbushe mchakato wa katiba mpya ulifanywa na tume ya Warioba na kina Polepole, Kabudi na wengine. Tume ya Warioba ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni na mapendekezo ya Katiba tuitakayo.

Kama wananchi tungekuwa hatutaki katiba mpya tusingetoa maoni na mapendekezo ya katiba tuitakayo kwa tume ya Warioba.

Kumbuka wewe ni kiongozi hivyo sio vema kupotosha ukweli chadema ina viongozi wanachama na wafuasi hao wote hao ni wananchi na wana haki ya kudai katiba mpya kama wananchi.
 
Katiba ya sasa haifai rais anaweza kuamua bunge liwe la chama kimoja, na kuwafanya wabunge wapitishe Sheria za kukandamiza wananchi mf. Tozo
 
Dawa ya hawa wanasiasa ni moja tu.

Mkutano wowote unaomhusu mwanasiasa ambaye ndiye mgeni rasmi. Nikunyanyua mabango kila kona yenye neno KATIBA na kutamka KATIBA.
 
Mbowe na genge lake waturudishie katiba yetu ambayo ilikuwa inaendana na jina na makusudia ya chama. Kukiita chama chetu "chadema" yani kirefu chama cha demokrasia na maendeleo tulikuwa tunamaanisha demokrasia ya kupokezana vijiti vya uongozi kwa kila baada ya miaka mitano mpaka kumi.

Sasa kitendo cha mwenyekiti wetu wa sasa kukinyofoa hicho kipande na kujimilikisha chama yeye mwenyew kwa muda usiojulikana, ni kuvunja kabisa miiko na dhumuni la kukiita chama chetu chama cha demokrasia. Lakini pia mwisho kuna neno linamalizika na maendeleo huku chama chetu chini ya huyu mwenyekiti aliejimilikisha chama, hatujaona maendeleo yoyote ya ofisi wala kichama.

Fikiria chama hakina mbunge wala ofisi ya maana. Inamaana hata kujenga ofisi nako tuilaumu tume ya uchaguzi na serikali ya ccm? Kama mwenyekiti, genge lake na chama kwa ujumla wameshindwa kujenga ofisi ya maana hili neno maendeleo limewekwa la nini?
 
Ni wananchi gani walisema kua WANATAKA CHADEMA wawe na Ofisi Mpya ili waweze kutatua matatizo yao
 
Hatusikii hatuoni kila kitakachotokea sasa hakitaweza kuupindisha umma wa WaTanzania walio wengi,matukio yote yanayokuja kwa kasi kama uyoga yatakufa kama uyoga.

Tanzania ya leo sio ile ya Mwalimu Nyerere ,wahusika msiache maCCM wakawachezea sharubu .
 
Hatusikii hatuoni kila kitakachotokea sasa hakitaweza kuupindisha umma wa WaTanzania walio wengi,matukio yote yanayokuja kwa kasi kama uyoga yatakufa kama uyoga,
Tanzania ya leo sio ile ya Mwalimu Nyerere ,wahusika msiache maCCM wakawachezea sharubu .
The constitutional reform as a current social need, is eminent and is in sight. It is just a matter of time.
 
Katiba na tume huru kwa sasa ndo vitaamua hatma ya Tanzania bora na imara
 
Hakika haiingii akili kumsikia katibu mkuu wa CCM eti anasema wananchi hawataki katiba mpya. Bw. Chongolo napenda nikukumbushe mchakato wa katiba mpya ulifanywa na tume ya Warioba na kina Polepole, Kabudi na wengine. Tume ya Warioba ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni na mapendekezo ya Katiba tuitakayo.

Kama wananchi tungekuwa hatutaki katiba mpya tusingetoa maoni na mapendekezo ya katiba tuitakayo kwa tume ya Warioba.

Kumbuka wewe ni kiongozi hivyo sio vema kupotosha ukweli chadema ina viongozi wanachama na wafuasi hao wote hao ni wananchi na wana haki ya kudai katiba mpya kama wananchi.
Ni kweli wananchi tunataka Katiba Mpya ILA si kwa mashinikizo na vitisho kama hivi kutoka kwa viongozi wa CHADEMA, ambao wote wanasukumwa na ulafi wa RUZUKU AU/NA POSHO watakazo pata wakati wa mchakato huo ambao wao wanataka uanzie tena Bungeni. Hii siyo sahihi, sisi wananchi tunataka tuanzie kwenye KURA YA MAONI - period. Hatua hii ndiyo sahihi na muafaka katika kutafuta Katiba Mpya, vinginevyo wasubiri kama alivyo sema Rais wetu SSH.
 
Mjumbe mmojawapo wa tume ya Warioba alikuwa Polepole!
Hakika haiingii akili kumsikia katibu mkuu wa CCM eti anasema wananchi hawataki katiba mpya. Bw. Chongolo napenda nikukumbushe mchakato wa katiba mpya ulifanywa na tume ya Warioba na kina Polepole, Kabudi na wengine. Tume ya Warioba ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni na mapendekezo ya Katiba tuitakayo.

Kama wananchi tungekuwa hatutaki katiba mpya tusingetoa maoni na mapendekezo ya katiba tuitakayo kwa tume ya Warioba.

Kumbuka wewe ni kiongozi hivyo sio vema kupotosha ukweli chadema ina viongozi wanachama na wafuasi hao wote hao ni wananchi na wana haki ya kudai katiba mpya kama wananchi.
 
Wakati mwingine tutakapoamua kuandika katiba mpya tume ya katiba iundwe na wataalamu tu wa katiba na sheria wenye umri kuanzia miaka 45 kutoka ndani na nchi za mbali zilizo na demokrasia ya juu.
 
Back
Top Bottom