GE2025 Wananchi Tunduru wagombea kadi za CHAUMMA kama 'njugu'

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Wananchi wa Tunduru, mkoani Ruvuma leo wamejikuta wakigombania kadi za kuomba uanachama wa Chama cha Ukombozi wa Umma(CHAUMMA).

Tukio hilo limetokea leo baada ya viongozi wa chama hicho kuzungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Tunduru.

Baada ya kumaliza kuzungumza, viongozi wa chama hicho walijikuta katika wakati mgumu baada ya idadi kubwa ya wananchi kuwakimbilia ili wapewe kadi za uanachama huku wengine wakivamia jukwaa.

Kutokana na hali hiyo iliwabidi viongozi wa chama hicho kuanza kuwaomba watulie na wasubiri kuwekewa utaratibu mzuri ili kila mtu apatiwe kadi ambapo wengine walifikia hatua ya kunyang'anyana kadi na kila aliyeipata alikwenda kupanga foleni kwa ajili ya kuandikisha jina kwa ajili ya kuomba kujiunga na chama hicho.

Acha bla blah.
Chauma na kadi za uwanachama wapi na wapi?
Chauma ni ubwabwa tu, wagawe ubwabwa watu watakimbilia na kupanga foleni, kadi za uanachama ni issue za Chadema, CCM nk.
 
erythrocyte atakataa
 
Ubwabwa walipika sufuria ngapi? 😹
 
Acha bla blah.
Chauma na kadi za uwanachama wapi na wapi?
Chauma ni ubwabwa tu, wagawe ubwabwa watu watakimbilia na kupanga foleni, kadi za uanachama ni issue za Chadema, CCM nk.
Ht macho hayaoni we bwege, chadomo kwishnet
 
Back
Top Bottom