- Source #1
- View Source #1
Taarifa zinadai kuwa kuna zoezi la ukusanyaji wa kodi ya mifugo linaendelea wilayani Ukerewe. Inadaiwa kuwa Mbuzi na Ng'ombe sasa wanalipiwa kodi. Yaonekana, kuna kodi nyingi zinarudishwa.
- Tunachokijua
- JamiiForums imefanya mawasiliano na viongozi wa Wilaya ya Ukerewe ili kupata ukweli wa madai haya ambao wameeleza yafuatayo:
Mkuu wa Wilaya, Kanali Denis Mwila anasema “Suala hilo mtafute Mkurugenzi ndiye atalizungumzia japokuwa ninavyojua hakuna tozo mpya ni zilezile zilizopo ambazo hazitungwi na Mkuu wa Wilaya wala Mkurugenzi."
“Zinatungwa na Serikali na wao ngazi ya chini wanatekeleza tu, lakini zungumza naye atakufafanulia.”
kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe bwana Emmanuel Luponya Sherembi anasema “Hakuna Tozo ni masuala ya herein, hilo ndilo linaloendelea na linafanyika kwa mujibu wa Sheria n ani maelekezo ya Serikali ili kupata utambuzi wa mifugo.
“Kuhusu kiasi cha malipo siwezi kukitaja kwa sasa kwa kuwa sina hizo takwimu lakini majibu ni hayo na linafanyika Nchi nzima.”