GE2025 Wananchi Vunjo wawashangaa wajumbe CCM kumnyima kura Dkt. Kimei

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

MTANZANIA620

Senior Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
105
Reaction score
116
Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Vunjo wameeleza mshangao wao mkubwa kufuatia kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Mhe. Dkt. Charles Kimei — ambaye amebaki kwenye kumbukumbu za wengi kama mbunge aliyetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kuliko watangulizi wake wote — hakupitishwa kuendelea kugombea.

Wakizungumza baada ya matokeo kutangazwa, baadhi ya wananchi walisema walitarajia uamuzi wa wajumbe ungefanyika kwa kuangalia rekodi ya utendaji na mchango katika maendeleo ya jimbo. Badala yake, kura zilimpeleka mbele mgombea kwa misingi ya rushwa, viongozi wa wilaya kumnadi na ambaye bado hajajijengea historia ya kujitegemea au uzoefu wa kutosha kuhusu changamoto na fursa zilizopo Vunjo.

Wananchi hao wamesema wanaamini vikao vya uteuzi vinauwezo wa kupata taarifa za ziada hivyo katika kulinda muendelezo wa maendeleo na kubadili siasa za Jimbo hili wataamua vinginevyo.
 
FB_IMG_1754455271266.jpg
 
Kwani yeye amefanya nini kinachoonekana zaidi?
Ni nani mbunge bora zaidi Tanzania? na amefanya nini cha ziada?
 
Wananchi wa maeneo mbalimbali ya Jimbo la Vunjo wameeleza mshangao wao mkubwa kufuatia kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ambapo Mhe. Dkt. Charles Kimei — ambaye amebaki kwenye kumbukumbu za wengi kama mbunge aliyetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo kuliko watangulizi wake wote — hakupitishwa kuendelea kugombea.

Wakizungumza baada ya matokeo kutangazwa, baadhi ya wananchi walisema walitarajia uamuzi wa wajumbe ungefanyika kwa kuangalia rekodi ya utendaji na mchango katika maendeleo ya jimbo. Badala yake, kura zilimpeleka mbele mgombea kwa misingi ya rushwa, viongozi wa wilaya kumnadi na ambaye bado hajajijengea historia ya kujitegemea au uzoefu wa kutosha kuhusu changamoto na fursa zilizopo Vunjo.

Wananchi hao wamesema wanaamini vikao vya uteuzi vinauwezo wa kupata taarifa za ziada hivyo katika kulinda muendelezo wa maendeleo na kubadili siasa za Jimbo hili wataamua vinginevyo.
Umetumwa si bure, kwanza Vunjo haina historia kubwa ya Mbunge kukaa mihula miwili. Pili huyu aliyeshinda, alifanya hivyo 2020 ila Kimei akabebwa na ushkaji wake na Hayati Magufuli. Leo Kimei kawa kimeo.
 
Back
Top Bottom