Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Wakuu leo nimeona huo Mjadala wa nchi kumi zenye bei kubwa zaidi ya mafuta umeibua hoja nyingi, lakini jambo moja lililokosekana ni ulinganisho wa mzigo halisi kwa wananchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Nimekutana na Takwimu mpya za Mei 2026 zinaonyesha kila nchi inatoboka tofauti kulingana na aina ya mafuta, na tofauti za bei zinafika zaidi ya shilingi elfu mbili kwa lita moja.
PETROLI
Rwanda ndiyo nchi raia wake wanatoboka zaidi kwenye petroli wakilipa TSh 5,223 kwa lita, ikifuatiwa na Kenya (TSh 4,319) na Tanzania (TSh 4,115). Chakushangaza kuna baadhi ya nchi karibu na jumuia walipa karibu ya nusu tu ya wastani wa bei za Afrika Mashariki , mfano Ethiopia ambapo mafuta ni nafuu zaidi kwa TSh 2,772 tu. Tofauti ya karibu ya shilingi 2,451 ikilinganishwa na Rwanda.
DIZELI
Kenya ndiyo inayoongoza Afrika Mashariki kwa bei kubwa zaidi kwenye mafuta ya dizeli, TSh 4,897 kwa lita Ikifuatia na Tanzania ambapo bila ya TSh 4,248 lita ya dizeli hupati, huku Rwanda ikilipa (TSh 3,465)
MAFUTA YA TAA
Kwenye bei ya mafuta ya Taa hapa Tanzania ndio tunaoumia zaidi. Wakuu hivi bado kuna watu wanatumia vibatali? Maana mradi wa REA umeshatekelezwa kwa zaidi Asilimia 99, Na vijiji zaidi ya 12,240 kati ya 12,318 vilivyo sajiliwa vimeunganishwa na umeme. Haya mafuta ya Taa anatumia nani? 🌚
Ila ninawasikitikia hao watumia mafuta ya Taa maana popote walipo wanatoboka TSh 4,677 kwa lita. Ni wazi huu ni mzigo mkubwa sana kama bado kutakuwa na familia zinazotegemea mafuta ya taa kwa kupikia na kuangazia😭
Kwa jumla, mzigo wa bei za mafuta kwa wananchi wa Afrika Mashariki ni mkubwa ukilinganisha na nchi jirani kama Ethiopia (nafuu kwa petroli na dizeli, lakini ghali kwa mafuta ya taa). Rwanda na Kenya zinaendelea kutathmini sera zao za mafuta ili kupunguza mzigo, huku Tanzania mwelekeo wa sera za ruzuku na kupunguza tozo zikikwepwa kwa kupendekeza Matumizi ya nishati mbadala na kupunguza misafara.
Mwigulu Nchemba (Waziri Mkuu)
Licha ya serikali kuonesha utayali wa kutaka kutua mzigo wa bei za mafuta, bado kuna suala huwa linakwepwa sana ambalo wananchi wanadhani ndio muarobaini wa kutua mzigo wa bei za mafuta. Huu si mwengine bali ni ule uliojikita kwenye Tozo zilizo ambatana na bidhaa za mafuta.
Kama unaacha watu wanapo jadili suala la tozo, Basi huu ni mkeka kipindi hiko lita ya petroli ilikuwa Tsh 2405
Kwa mwenendo wa mchanganuo wa bei hizo za julai 2021 ni wazi kuwa kama kutakuwa hakuna tozo mpya iliyoongozwa basi ile bei ya Petrol kwa wakazi wa Dar es salaam (Tsh 4,115) kama ingetolewa makoto yote, ingekuwa Tsh 2,127.45 tu, Kitu baadhi ya watu wanadhani ni suala lililopo ndani ya uwezo wa serikali hata kama sio kuondoa mzigo wote makato, lakini angalau hata Tsh 1000 ingewezekana.
Wakuu nawasilisha🙏🏾
Vyanzo rasmi:

Sisi tuna gesi yetu na vifaa vingi vinatumia gesi maana yake hatutaathirka sana panapotokea matatizo kama haya kwenye nchi zinazo zalishamafuta.
Licha ya serikali kuonesha utayali wa kutaka kutua mzigo wa bei za mafuta, bado kuna suala huwa linakwepwa sana ambalo wananchi wanadhani ndio muarobaini wa kutua mzigo wa bei za mafuta. Huu si mwengine bali ni ule uliojikita kwenye Tozo zilizo ambatana na bidhaa za mafuta.
Kama unaacha watu wanapo jadili suala la tozo, Basi huu ni mkeka kipindi hiko lita ya petroli ilikuwa Tsh 2405
Kwa mwenendo wa mchanganuo wa bei hizo za julai 2021 ni wazi kuwa kama kutakuwa hakuna tozo mpya iliyoongozwa basi ile bei ya Petrol kwa wakazi wa Dar es salaam (Tsh 4,115) kama ingetolewa makoto yote, ingekuwa Tsh 2,127.45 tu, Kitu baadhi ya watu wanadhani ni suala lililopo ndani ya uwezo wa serikali hata kama sio kuondoa mzigo wote makato, lakini angalau hata Tsh 1000 ingewezekana.
Wakuu nawasilisha🙏🏾
Vyanzo rasmi:
- EWURA Tanzania – Cap Prices May 2026
- EPRA Kenya – Fuel Prices May 2026
- RURA Rwanda – Fuel Tariffs
- Ethiopian Ministry of Trade – Fuel Price Updates
- GlobalPetrolPrices – Uganda Fuel Prices
- The Chanzo - Majibu ya Mwigulu