Wananchi wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga, linaloongozwa na Mbunge Januari Makamba, wameeleza shukrani zao kwa Serikali kwa kuwafikishia miradi mbalimbali ya maendeleo kupitia mbunge wao, ikiwemo huduma za umeme, maji, na ujenzi wa zahanati.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wananchi hao wameeleza kuwa Bumbuli ya sasa imepiga hatua kubwa ikilinganishwa na miaka iliyopita, huku wakimsifu Makamba kwa usimamizi thabiti wa miradi ya maendeleo.
“Tumefanya tathmini, hakuna mtu wa kukutoa hapa. Ubunge labda uache wewe mwenyewe tu, lakini Bumbuli ya mwaka 2010 sio Bumbuli ya leo. Tumepata maendeleo makubwa sana,” amesema mmoja wa wakazi wa eneo hilo.