Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Wananchi wa Jimbo la Manonga wameeleza kuumizwa na kitendo cha aliyekuwa Mbunge wao, Seif Hamisi Gulamali, kutorejea tena kugombea Ubunge katika jimbo hilo.
Wakizungumza kupitia taarifa ya makala maalum, wananchi hao wameeleza kuwa jina la Gulamali limeacha alama kubwa ya kisiasa na maendeleo, kwani katika kipindi cha miaka kumi ya uongozi wake alileta mabadiliko makubwa katika jimbo hilo jipya lililoanzishwa mwaka 2015.
Gulamali ndiye Mbunge wa kwanza wa Jimbo la Manonga na alifanikiwa kuliongoza kwa miaka kumi mfululizo, akiwakilisha wananchi kwa juhudi kubwa za kuwaletea maendeleo katika sekta mbalimbali elimu, afya, maji, miundombinu na nishati.