Pre GE2025 Wananchi wa Kijiji cha Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba, waishukuru serikali kwa kuwajengea shule ya sekondari

Pre GE2025 Wananchi wa Kijiji cha Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba, waishukuru serikali kwa kuwajengea shule ya sekondari

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Wananchi wa Kijiji cha Mtyangimbole kata ya Mtyangimbole Halmashauri ya Madaba, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Mbunge wa Jimbo la Madaba Joseph Kizito Mhagama, kwa kujenga shule ya sekondari katika eneo hilo ambayo imeondoa adha kubwa iliyokuwa ikiwakumba wanafunzi kulazimika kutembea umbali mrefu wa zaidi ya kilomita nne kufuata elimu, na hivyo kuongeza muda wa kupumzika na kujisomea kwa wanafunzi.

Kwa mujibu wa Jackson Lomanus Luambano Mkazi wa Kijiji cha Mtyangimbole, ujenzi wa shule ya sekondari umeleta faraja kubwa kwa jamii kwani wanafunzi sasa wataweza kupata elimu bora katika mazingira bora, huku wananchi wakitoa pongezi kwa Rais Samia kutoa kipaumbele katika sekta ya elimu ambayo imekuwa chachu ya maendeleo katika jimbo hilo.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Yolanda Ngonyani , amesema kuwa watoto wao walikuwa wanapata shida kubwa kwenda shuleni Nguruma, ambapo walilazimika kubeba mabegi mazito na kutembea umbali mrefu Hali hiyo ilikuwa ikiwachosha na mara nyingi walikuwa wakishindwa kushiriki kazi za nyumbani kutokana na uchovu wa kutembea umbali mrefu.
Screenshot 2025-02-19 150332.png
 
Back
Top Bottom